Yanga SC
YANGA SC YAJA KWA KASI YAO, ZIMBWE JR ASEMA SIMBA SIO TATIZO
Vardo
May 24, 2026
10:01 am
BEKI wa pembeni wa Yanga SC, Mohammed Hussein ‘Zimbwe JR’, amesema hakuna presha yoyote ndani ya kikosi hicho kutokana na kasi inayoonyeshwa na wapinzani wao Simba SC.
Amesisitiza kuwa malengo yao ni moja tu, kusaka alama tatu katika kila mchezo wanaocheza.
Zimbwe JR amesema Yanga SC wanaendelea kufanya kazi kwa utulivu mkubwa na hawaruhusu ushindani wa ligi kuwatoa kwenye malengo yao ya msingi, ambayo ni kuhakikisha wanashinda kila mechi na kubeba mataji yote wanayoshiriki msimu huu.
Amefafanua kuwa ndani ya kikosi hicho kila mchezaji anaelewa wajibu wake, huku wakibaki imara kisaikolojia licha ya presha ya ushindani mkali wa kuwania ubingwa dhidi ya wapinzani wao wakubwa Simba SC.
Akizungumzia hali yake ya majeruhi, beki huyo amesema anaendelea vizuri na ana imani muda si mrefu atarejea uwanjani kuendelea kuisaidia timu yake katika majukumu ya msimu huu.
“Namshukuru, naendelea vizuri. Nina imani nina muda mfupi tu nitarudi katika majukumu yangu,” amesema Zimbwe JR, akionyesha matumaini ya kurejea haraka kwenye kikosi cha kwanza.
Ameongeza kuwa kikosi cha Yanga SC kipo katika mstari mzuri wa ushindani wa mataji mbalimbali, huku wakilenga kubeba kila kombe linalowezekana ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la CRDB.
“Kikubwa lazima tufikishe malengo kila msimu, kushinda kila kombe. Kuna CRDB na Ligi, hadi sasa tupo vizuri,” ameongeza, akisisitiza uimara wa timu hiyo katika mbio za ubingwa wa msimu huu.