Michezo Bongo

MALINDI YAHITAJI MIUJIZA KUBAKI ZPL

Vardo May 29, 2026 9:01 pm

HALI iliyonayo Malindi hivi sasa inahitaji maombi kuona inasalia Ligi Kuu Zanzibar kutokana na kupoteza mechi mbili za karibuni dhidi ya Polisi (3-0) na Muembe Makumbi (3-1).

Katika mechi iliyochezwa Mei 22 mwaka huu, Polisi iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Malindi huku Muembe Makumbi ikiitoa nje ya matumaini ya kubaki ZPL baada ya kuitembezea kichapo cha mabao 3-1, Mei 26, 2026.

Baada ya Malindi kupoteza mechi hizo mfululizo, imeonekana kuwa na hali mbaya zaidi katika msimamo wa ZPL ikipambana kujinasua kutoka katika mstari wa kushuka daraja kuzifuata New Stone Town na Junguni..

Malindi ni miongoni mwa timu zilizoanza vizuri msimu huu na kutabiriwa kuwa miongoni mwa zitakazobeba ubingwa wa ligi hiyo, ndoto hizo ziliishia njiani mara tu uongozi wa timu hiyo kuvurugika.

Kwasasa timu hiyo inahitaji miujiza ya kubaki Ligi Kuu Zanzibar kwani Polisi ambayo ilikuwa ikichuana na timu hiyo imeanza kupata matumaini baada ya kuibuka na ushindi zilipokutana.

Malindi kwa sasa imebakiwa na mechi tatu dhidi ya Zimamoto, New King na Kipanga ambapo New King inapambana isishuke daraja, huku Kipanga na Zimamoto zikiwa kwenye vita ya kumaliza nne bora.

Katika msimamo wa ZPL, Malindi inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 27. Ipo ndani ya timu nne zinazotakiwa kushuka ambapo sasa nafasi zimebaki mbili baada ya New King na Junguni kushuka.

RATIBA YAMUIBUA KOCHA MUEMBE MAKUMBI SABABU YA LINGARD KUITWA JLINGZ YAFICHUKA