Habari za michezo

Yanga Yapata Nafuu, FIFA Yaiondolea Adhabu Ya Usajili

Vardo July 14, 2026 7:05 pm

HII ni habari njema kwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, baada ya kuondolewa adhabu ya kuzuiwa kusajili wachezaji iliyokuwa imewekwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kufuatia klabu hiyo kukamilisha kushughulikia kesi iliyokuwa ikiikabili.

Kuondolewa kwa adhabu hiyo kunatoa nafuu kubwa kwa Yanga, ambao sasa wako huru kusajili na kuwaandikisha rasmi wachezaji wapya kuelekea maandalizi ya msimu wa 2026/27.

Awali, Yanga ilikuwa imewekewa zuio la usajili kutokana na kesi iliyokuwa mbele ya FIFA, jambo lililozua wasiwasi miongoni mwa mashabiki kuhusu uwezo wa klabu hiyo kuimarisha kikosi kwa wakati kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Hata hivyo, baada ya kumaliza suala hilo na kuondolewa kwa adhabu hiyo, uongozi wa klabu sasa unaweza kuendelea na mipango ya kukamilisha usajili wa nyota waliowalenga kwa ajili ya kuimarisha kikosi.

Hatua hiyo pia inafungua ukurasa mpya kwa Yanga katika maandalizi ya msimu wa 2026/27, ikipewa nafasi ya kujenga kikosi chenye ushindani kitakachowania kutetea mataji ya ndani na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Chuga Boy Aipa Kisogo KAA Gent,  Kisa Mamillion Ya Yanga Usajili Mzito Yanga! Flomo Asubiri Baraka Za Al Hilal