Simba SC

Ratiba Kamili Simba Day 2026: Uzinduzi Wa Jezi Mpya, Marathon Na Kilele Uwanja Wa Uhuru

Vardo July 20, 2026 12:18 pm

Wakati maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2026/27 yakipamba moto, klabu ya Simba SC imeweka wazi ratiba kamili ya matukio kuelekea tamasha kubwa la Simba Day 2026, linalotarajiwa kufanyika Agosti 8 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, mfululizo wa shughuli hizo utaanza rasmi Julai 25 kwa uzinduzi wa kampeni za Simba Day, hafla inayotarajiwa kuwaleta pamoja viongozi, wanachama, mashabiki na wadau mbalimbali wa michezo.

Matukio Makuu Kuelekea Simba Day 2026:

  • Julai 25 – Uzinduzi Rasmi wa Simba Day: Mwanzo wa shughuli na hamasa kote nchini.

  • Agosti 1 – Uzinduzi wa Jezi Mpya (2026/27): Simba itatambulisha uzi mpya watakaoutumia msimu ujao, tukio linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki ili kuona muonekano na ujumbe mpya wa klabu.

  • Agosti 2 – Simba Marathon: Mbiyo maalumu zitakazowakusanya maelfu ya wanembo na mashabiki kwa ajili ya kuhamasisha afya, mshikamano, pamoja na kuendelea kuikuza chapa ya Simba SC.

  • Agosti 8 – Kilele cha Simba Day (Uwanja wa Uhuru): Tamasha kubwa la kilele litakaloshuhudia utambulisho wa kikosi kipya cha msimu wa 2026/27, wachezaji wapya waliosajiliwa, benchi la ufundi, pamoja mechi ya kirafiki na burudani za wasanii mbalimbali.

Uongozi wa Simba unaendeleza utamaduni wake wa kufanya Simba Day kuwa zaidi ya mchezo wa mpira wa miguu, ukitoa fursa kwa mashabiki kushiriki matukio ya kijamii na michezo ili kujenga hamasa kabla ya kuanza rasmi kwa msimu mpya.

UFC Fight Night Serbia: Meridianbet Yaandika Historia Belgrade! Yanga Yamaliza Usajili 2026/27: Yaahidi Utambulisho Wa ‘Ghafla Bin Vuu’