Eng. Hersi Said Atoa Wito Mzito Kwa Wanachama Wa Yanga Baada Ya Uchaguzi
Rais wa klabu ya Yanga SC, Injinia Hersi Said, amewataka kwa dhati wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuvunja mara moja makundi na kambi zote za uchaguzi zilizoundwa wakati wa mchakato wa kuchagua viongozi wapya.
Hersi ameyasema hayo wakati akihutubia Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Yanga uliofanyika Agosti 2, 2026, na kukamilika usiku wa kuchia leo.
“Wagombea Waliokosa Nafasi Sio Maadui” — Hersi Said
Akitangaza mwelekeo mpya baada ya kutetea kiti chake cha Urais, Injinia Hersi amesisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi hayapaswi kuleta chuki au mpasuko miongoni mwa wanachama na wagombea walioshindwa.
“Niwapongeze kwa dhati wagombea wote waliofanikiwa kuingia kwenye Kamati ya Utendaji — nawaona watatu wa zamani waliorejea na wawili wapya, karibuni sana tuwatumikie wana-Yanga,” amesema Hersi.
“Lakini pia, wagombea ambao hawajafanikiwa kupata kura za kutosha bado ni washindi na ni sehemu muhimu ya Yanga. Hawatakiwi kugeuka maadui wa klabu yetu. Hapa hakuna aliyeshindwa, wote ni wanachama na tunawahitaji kwenye safari hii.”
Wanachama Watakiwa Kuunganisha Nguvu
Aidha, Rais Hersi ametoa rai kwa wanachama kote nchini kuweka pembeni tofauti zao na kurudisha nguvu ya umoja ili kuijenga Yanga thabiti kwa miaka minne ijayo.
“Wanachama wenzangu, nawataka mvunje kambi zote huko mitaani na kwenye matawi. Mtu wako akiwa ameshinda au ameshindwa, nyote ni wanachama wa Yanga na sio wa mtu binafsi. Turudi pamoja kuunganisha nguvu zetu na kuipigania klabu yetu,” aliongeza.
📋 Safu Mpya Ya Uongozi Wa Yanga SC
Katika uchaguzi huo, safu mpya ya uongozi itakayoongoza Wananchi kwa miaka minne ijayo inaundwa na:
-
Rais: Eng. Hersi Said
-
Makamu wa Rais: Arafat Haji
-
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji:
-
Yanga Makaga
-
Alexander Ngai
-
Munir Seleman
-
Julius Koyi
-
Fahd Afif
-