Simba SC Ligi ya Mabingwa
Simba SC

Simba SC Yocha Mighty Wanderers 6-1: Mkwabi Aagiza Azam FC Wakae Tayari!

Vardo September 14, 2026 10:30 am

Mkwabi Aipongeza Simba SC Baada ya Kipigo cha 6-1, Aipiga Bit Azam FC Mchezo Ujao

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Simba SC, Swed Mkwabi, amemwagia sifa tele Kocha Mkuu Steve Barker pamoja na benchi lake lote la ufundi baada ya timu hiyo kuonyesha kiwango cha kimataifa na kupata ushindi mnene kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba SC iliiadhibu Mighty Wanderers ya Malawi kwa kuichapa mabao 6-1 katika mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Ushindi huo uliifanya Simba kufuzu hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 7-1 (Aggregate).

Akiashiria kuridhishwa na kiwango hicho, Mkwabi alisema:

“Steve Barker na benchi lake tunawapongeza sana. Wamefanya kazi kubwa sana katika timu. Tumetofautiana na tumewashinda. Tuwapongeze wachezaji, wamefanya vizuri.”

Mashabiki Wamwagiwa Sifa Tele

Mkwabi hakusita kuwashukuru mashabiki wa Simba SC waliojitokeza kwa wingi uwanjani, akieleza kuwa ushabiki na sapoti yao imekuwa chachu kubwa ya matokeo hayo mazuri.

“Mashabiki tunawashukuru sana wote. Timu imeonyesha kuwa na kiwango cha juu sana, kuanzia mchezo wa kwanza hadi mchezo wa pili. Sisi kama viongozi tumefurahi sana na kile ambacho tumejiandaa,” aliongeza Mkwabi.

Focus Ni Kimataifa na Ligi Kuu

Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa malengo makubwa ya Simba SC ni kufanya vizuri kimataifa huku wakidumisha hamasa ya ushindi katika kila mchezo unaowakabili.

Mpaka sasa, Simba SC ipo kwenye muendelezo mzuri wa matokeo baada ya kushinda mechi zake zote mbili za Ligi Kuu pamoja na michezo yote miwili ya awali ya kimataifa.

Kipanya Kipya Kinaelekezwa Kwa Azam FC

Baada ya kukamilisha salama kibarua cha kimataifa, Mkwabi amewataka wachezaji na benchi la ufundi kuelekeza nguvu zote kwenye mchezo unaofuata wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC, akiahidi kuwa wamejipanga kuondoka na pointi tatu muhimu.

“Ni mechi ngumu. Azam ni timu nzuri, lakini na sisi tutaibuka na ushindi kutokana na mipango tuliyonayo na mwalimu pamoja na timu,” alimalizia Mkwabi.

Mangungu Aitumia Ujumbe Mzito Afrika Baada ya Simba Kushinda 6-1 Vita Ya Makundi CAF: Ratiba Na Wapinzani Wa Simba, Yanga, Azam Na Singida BS