Simo Dladla Yanga SC
Habari za michezo

Simo Dladla Afichua Eneo Yanga Inalotakiwa Kurekebisha Haraka Baada ya Kuichapa St George

Vardo September 20, 2026 8:33 am

Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Simo Dladla, amefichua eneo nyeti ambalo Mabingwa hao watetezi wanapaswa kulifanyia kazi kwa haraka zaidi, kufuatia ushindi wa bao 1-0 walioupa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya St George ya Ethiopia.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, bench la ufundi la Yanga lilitumia fursa hiyo kuwapa wachezaji muda wa kucheza ili kuongeza utimamu wa mwili na kuimarisha uelewano wa mbinu za timu.

Dladla ameeza kuridhishwa na kiwango cha timu katika kumiliki mpira na kuzuia nafasi, lakini akasisitiza kuwa makali ya safu ya ushambuliaji bado yanahitaji maboresho makubwa.

“Kwa maoni yetu, tulitawala mchezo kikamilifu. Lengo letu lilikuwa kumiliki mpira na kuzuia mianya pale ambapo hatukuwa na mpira. Kila tulipopoteza mpira, wachezaji walifanya pressing na counter-pressing kwa haraka ili kurudisha mpira mikononi mwetu,” alisema Dladla.

Hata hivyo, Kocha Dladla amebainisha kuwa bado kuna changamoto katika eneo la mwisho la ushambuliaji (final third).

“Eneo la mwisho bado linahitaji kazi ya ziada. Ni vigumu kutarajia wachezaji ambao hawajacheza mechi nyingi kuwa na makali ya juu mara moja, lakini hilo ni eneo linalopaswa kufanyiwa kazi kwa karibu zaidi,” aliongeza.

Pia alibainisha kuwa ingawa Yanga ilitawala sehemu kubwa ya mchezo, haikuweza kupenya mstari wa ulinzi wa St George mara nyingi kama walivyopanga. Licha ya hayo, bench la ufundi limeridhishwa na mwenendo mzima wa kikosi hicho katika mchakato wa kujiweka sawa kwa ajili ya mechi rasmi zinazofuata.

Erik Mwijage Aanza Na Moto Yanga: Aweka Wazi Mipango Yake Na Ushindani Wa Namba!