Simba SC dhidi ya Yanga
Yanga SC

Rushine De Reuck Aivulia Kofia Kambi ya SA: “Simba Ipo Tayari Kuifunga Yanga Dabi ya Kariakoo”

Vardo October 5, 2026 10:12 am

NAHODHA na mlinzi wa kati wa Simba SC, Rushine De Reuck, ameweka wazi kuwa kambi ya siku 10 waliyoifanya nchini Afrika Kusini imekuwa chachu kubwa ya kukiandaa kikosi chao kiakili na kimwili kuelekea mchezo wa Simba SC dhidi ya Yanga.

Simba itakuwa mwenyeji wa watani wao wa jadi, Yanga, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kupigwa Jumamosi, Oktoba 10, 2026. Mchezo huo unafahamika kama Dabi ya Kariakoo, ambapo tayari presha na hamasa kubwa zimeanza kutawala miongoni mwa mashabiki wa soka nchini.

De Reuck, ambaye anatarajiwa kuwa mhimili mkuu katika safu ya ulinzi ya Wekundu wa Msimbazi, amebainisha kuwa mazingira yenye ushindani mkubwa waliyokutana nayo Afrika Kusini yamewajenga wachezaji wote na kuongeza utayari wao wa kukabiliana na ratiba ngumu inayowasubiri.

“Kipindi chote cha maandalizi kimetupa fursa ya kufanya kazi kwa pamoja kama timu. Kila mchezaji ameonyesha maendeleo makubwa na kiwango kinachotupa matumaini ya kufanya vizuri zaidi msimu huu,” alisema De Reuck.

Beki huyo raia wa Afrika Kusini aliongeza kuwa kambi hiyo imekuwa na faida kubwa kwani imewapa wachezaji wengi muda wa kucheza, kuonyesha uwezo wao, na kupigania namba katika kikosi cha kwanza—jambo lililoongeza ushindani wa namba kikosini.

Akizungumzia pambano hilo la Simba SC dhidi ya Yanga, De Reuck amesisitiza kuwa kikosi kizima kipo tayari na wachezaji wana hamu kubwa ya kuingia uwanjani ili kuwapa furaha mashabiki wao katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mamilioni ya wapenda soka.

“Dabi Haina Friendship, Ni Do or Die!” – Simba Yaweka Wazi Mipango Yote Dhidi ya Yanga Ally Kamwe Afunguka Mazito Kuelekea Dabi ya Yanga vs Simba | Ligi Kuu