Home Habari za michezo AHMED ALLY:- USAJILI WA KIBU DENIS ULITUTESA SANA…ALIKUWA ANAPITA HUKU ANATOKEA KULE…

AHMED ALLY:- USAJILI WA KIBU DENIS ULITUTESA SANA…ALIKUWA ANAPITA HUKU ANATOKEA KULE…

Kibu denis Simba

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa hakuna usajili ambao uliwatetesa viongozi hao kama ule wa kiungo mshambuliaji wao, Kibu Denis.

Kauli hiyo ya Ahmed imekuja ikiwa ni siku chache baada ya mchezaji huyo kugoma kujiunga na kambi ya klabu huko Misri na kutimkia nchini Norway ambako anadaiwa kupata dili.

“Hakuna usajili uliotutesa Simba kama wa kumuongezea mkataba Kibu Denis. Alikuwa anasema ntaongeza mkataba, ntaongeza mkataba Anapitia huku anatokea huku. Wavimba macho nao walikuwa wanamvizia Hatukulala wiki mbili.

“Watu wanasema ana goli moja. Ndio ana goli moja lakini anajituma sana. Kibu ni aina ya wachezaji ambao wanacheza kama timu za baba zao, Hakuna timu inatamani kukutana na Kibu,” amesema Ahmed Ally.

KLABU YATOA TAARIFA.

Wakati taarifa zikienea kiungo mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis amekimbilia Norway, uongozi wa klabu hiyo umesema utamchukulia hatua za kinidhamu ikidai ni mtoro.

Kauli ya Simba inakuja baada ya kuibuka kwa taarifa Kibu ametimkia Norway kimya kimya bila kutoa taarifa kwa klabu yake.

Simba imezinasa nyaraka mbalimbali za Kibu zikionyesha kiungo huyo ametimka nchini na sasa inafanya mawasiliano na uongozi wa mchezaji huyo.

Sakata hilo limeibuka baada ya kiungo huyo kuzusha sintofahamu ya kutorejea kazini, tangu asaini mkataba mpya wa miaka miwili kisha kutimkia Marekani kwa mapumziko ya mwisho wa msimu.

Hata aliporejea nchini akitokea Marekani, Kibu hakujiunga na timu hiyo licha ya uongozi wa Simba kupitia Meneja wa Habari, Ahmed Ally kuthibitisha klabu yao imechukua hatua nyingi za kumsaka ili akajiunge na wenzake kwenye kambi yao iliyoko jijini Ismailia, Misri.

Simba kwa sasa iko Ismailia ilikoweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, huku mchezaji huyo hadi sasa bado hajaripoti na taarifa zinadai ametimkia Norway.

Taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo leo Julai 23 , imeeleza sababu za mchezaji huyo kitojiunga na kambi ya timu hiyo hadi sasa.

“Klabu ya Simba inautaarifu umma, mchezaji wake Kibu Denis Prosper hajaripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2024-2025.”

“Tunapenda kuutarifu umma, Simba tulimwongezea mkataba Kibu wa miaka miwili zaidi utakaoisha Juni 2026 na kumlipa stahiki zake zote za kimkataba,” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza;

“Hata hivyo mchezaji huyu amekuwa akitoa sababu kadha wa kadha zinazomfanya kushindwa kuripoti kambini na kutokana na utovu huu wa nidhamu, klabu itamchukulia hatua stahiki za kinidhamu na umma utapewa taarifa,” mwisho wa kunukuu taarifa hiyo.

SOMA NA HII  WALA SIMBA HAIWAOGOPI AZAM HATA KIDOGO