ISHU YA RAIS WA BARCELONA KUBWAGA MANYANGA, MESSI ATAJWA
KLABU ya Barcelona imetangaza rasmi aliyekuwa Rais wao, Josep Maria Bartomeu, amejiuzulu nafasi hiyo pamoja na bodi yote ya wakurugenzi. Bartomeu, 57, amekuwa Rais wa Barcelona tangu mwaka 2014, lakini homa ya kuachia kiti hicho iliongezeka majira ya kiangazi mwaka huu baada nyota wa timu hiyo, Lionel Messi, na wachezaji wengine wa Barcelona kukosoa hadharani uongozi wake hasa klabu hiyo...
ABDI BANDA YUPO ZAKE BONGO, TIMU YAKE YAUZWA
BEKI wa zamani wa Simba ambaye anakipiga ndani ya Highland Parks FC ya nchini Afrika Kusini, Abdi Banda amerejea nchini kwa mapumziko mafupi baada ya timu yake kuuzwa na kubadilishwa jina na kuitwa Ts Galaxy. Akizungumza na Saleh Jembe Banda amesema kuwa mwisho wa mwezi wa kumi alipigiwa simu na uongozi wa timu ya Ts Galaxy, ili waweze kumtumia tiketi...
OKTOBA INA MENGI KINOMA, SIMBA YALAMBISHWA SHUBIRI
NI hesabu za vidole tu ambazo unaweza kuzifanya wakati ambao unataka kuubadilisha mwezi Oktoba kwenda ule unaofuata wa Novemba. Huu ni mwezi wapili wa mwisho wa mwaka.Mwezi Oktoba unaondoka ukiwa na mambo mengi kuanzia ya kijamii, siasa na hata muziki. Kama umesahau nakukumbusha leo Jumatano ndiyo Watanzania wanapiga kura kuchagua marais, wabunge na madiwani.Pia mwezi huu katika upande wa...
KAZE WA YANGA AACHWE AFANYE KAZI KWA SASA
KLABU ya Yanga kwa sasa ipo chini ya kocha mpya, Cedric Kaze ambaye tayari amesimamia mechi mbili za ligi na kushinda zote dhidi ya Polisi Tanzania (1-0) na KMC (1-2). Yanga kwa sasa katika msimamo kwa ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 19 tu baada ya mechi saba na hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa. Na huu ndiyo mwanzo wa Kaze...
NAHODHA WA SIMBA BOCCO AOKOLEWA KUPIGWA MAWE NA POLISI KUTOKA KWA MASHABIKI
KATIKA hali ya kushangaza mshambuliaji wa Simba, John Bocco, juzi alinusurika kupigwa na mawe na mashabiki wa timu hiyo kufuatia kitendo cha kukosa penalti katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambao walichapwa bao 1-0. Bocco alikosa penalti dakika ya 78 kwa shuti lake kugonga mwamba hali ambayo iliwakasirisha mashabiki kwa kuwa mchezo uliopita walifungwa bao 1-0...
KLOPP HAELEWI CHA KUFANYA KUHUSU NAFASI YA ULINZI
JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu kuhusu uimara wa safu yake ya ulinzi baada ya beki wake mwingine Fabinho Tavares kuumia kwenye kipindi cha kwanza wakati wakipambana na Midtylland usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Anfield.Raia huyo wa Brazili alikuwa anaziba nafasi iliyokuwa inachezwa na beki kisiki wa timu hiyo Virgil van Dijk...
MAMBO MAZITO BAADA YA LIGWARIDE SIMBA,WANNE WAFUTWA KAZI
IMEELEZWA kuwa Klabu ya Simba imewafuta kazi Mwarami Mohamed (Kocha wa magoli kipa) na Patrick Rweyemamu (Meneja wa timu ) kutokana na matokeo mabaya kwa mechi mbili Mfululizo Simba imecheza mechi mbili mfululizo na kupoteza pointi sita ambapo ilianza kufungwa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela na ikachapwa tena bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja...
CIOABA WA AZAM FC NA SVEN WA SIMBA WANYOOSHWA NA WAZAWA
TARATIBU mbinu za wazungu zinaanza kufeli mbele ya wazawa ambao wanazinoa timu zao kwa kubeba pointi tatu mbele ya makocha wakigeni.Oktoba 22, Tanzania Prisons inayonolewa na mzawa Salum Mayanga alikiongoza kikosi chake kuitungua Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji.Kwenye mchezo huo Prisons ilishinda bao 1-0 dhidi ya Simba Uwanja wa Nelson Mandela, Oktoba 26, Simba...
KUMBE KOCHA SIMBA HAJUI SABABU YA VIPIGO KUTOKA KWA WAJEDA
SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa bado hajajua sababu ya kupoteza mechi mbili mfululizo jambo ambalo linampa tabu katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.Wakiwa ni mabingwa watetezi wameyeyusha jumla ya pointi nane ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21 baada ya kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na ilipoteza mechi mbili ilikuwa mbele...
RUVU SHOOTING: TULIWAAMBIA SIMBA MAPEMA KWAMBA TUTAWAPAPASA, WALIPUUZA
OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa aliwapa tahadhari mapema wapinzani wake Simba kabla ya kukutana nao uwanjani jambo ambalo walilipuuzia awali.Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Oktoba 26, Uwanja wa Uhuru Simba ilikubali kichapo cha bao 1-0 na kuyeyusha pointi tatu wakiwa nyumbani.Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema kuwa taarifa za kuwapapasa alizitoa mapema ila...