VIGONGO VITANO VYA MOTO KWA SIMBA ACHA KABISA, YANGA NDANI
BAADA ya Oktoba 31 Simba kuifunga kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mwadui FC ndani ya Novemba ina kazi ya kusaka pointi 15 kwa kuwa itamenyana na timu tano ndani ya uwanja. Kazi kubwa itakuwa ni kusaka pointi sita ikiwa nyumbani mbele ya Kagera Sugar na KMC.Pointi tisa itasaka ikiwa ugenini ambapo ni mbele ya Yanga, Coastal Union na...
POGBA: NILIFANYA KOSA LA KIJINGA NDANI YA UWANJA
KIUNGO wa kati wa Manchester United, Paul Pogba, amekubali kupokea lawama baada ya kucheza rafu dhidi ya mchezaji wa Arsenal, iliyosababisha penati ambayo iliamua matokeo ya mchezo huo wa ligi kuu ya England. Pogba alinyanyua mguu uliomuangusha Hector Bellerin ndani ya eneo la hatari na Pierre-Emerick Aubameyang akafunga bao lililoipa ushindi Uwanja wa Old Trafford. ”Tunajua kwamba kilikuwa ni kiwango duni,...
LUSAJO NYOTA WA KMC ALIYEIBUKIA KUTOKA NAMUNGO ATAJA MABAO ATAKAYOFUNGA
MSHAMBULIAJI wa KMC, Relliants Lusajo, ameweka wazi kuwa mikakati yake msimu huu ni kuifungia timu hiyo mabao yasiyopungua 15 katika Ligi Kuu Bara, huku akiamini yataisaidia timu hiyo kufanya vizuri. Lusajo amejiunga na KMC msimu huu akitokea Namungo ambapo msimu uliopita alimaliza ligi akifunga mabao 13, huku msimu huu akiwa na KMC amefunga mabao matatu katika michezo mitano aliyoichezea timu...
BERNARD MORRISON NA SHOMARI LAWI WANATUACHIA MASWALI MAGUMU
LILIKUWA suala la muda tu kabla ya kuisikia hukumu ya mchezaji aitwaye Bernard Morrison. Tulikuwa na hakika kuwa atakumbana na adhabu baada ya kamera kumnasa akimpiga ngumi beki wa Ruvu Shooting, Juma Said Nyoso.Kikao cha Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), kilikaa tarehe 27 Octoba na kutoa adhabu kwa wachezaji na timu zilizovunja sheria. Hakuna aliyejali sana kuhusu adhabu...
MANCHESTER UNITED WANATIA HURUMA, WAKUSANYA MABAO 10
MANCHESTER United imeshuhudia maumivu tena ikiwa Uwanja wa Old Trafford kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu England na kufanya ikusanye jumla ya mabao 10.Bao pekee la ushindi kwa Arsenal inayonolewa na Mikel Arteta lilipachikwa kimiani na nahodha wao raia wa Gabon, Pierre Emerick Aubameyang dakika ya 69 kwa mkwaju wa penalti uliosababishwa na...
AZAM FC YAIPIGIA HESABU DODOMA JIJI FC
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC wameanza kuipigia hesabu Dodoma Jiji kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi utakaochezwa Novemba 5, Uwanja wa Azam Complex.Azam FC ikiwa imecheza jumla ya mechi 9 imejikusanyia pointi 22 inakutana na Dodoma Jiji ambayo imecheza mechi 9 na kujikusanyia pointi 12 ikiwa nafasi ya 10.Mchezo wao uliopita Azam FC ililazimisha sare ya...
LIGI KUU BARA HIZI HAPA UWANJANI
LEO Novemba 2 ulimwengu wa Ligi Kuu Bara unaendelea ambapo mchezo mmoja utachezwa kwa timu mbili kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.Uwanja wa Sokoine dakika 90 za moto nyasi zitawaka kwa kushuhudia miguu ya wanaume 22 wakipambana kuonyeshana umwamba.Mbeya City ambayo imecheza jumla ya mechi 8 na kujikusanyia jumla ya pointi 5 inawakaribisha Ihefu FC ambao wamecheza jumla ya...
KMC YATUMA SALAMU KWA BIASHARA UNITED
UONGOZI wa Klabu ya KMC umesema kuwa kwa sasa utaendelea kushusha dozi kwa kila timu itakayokutana nayo kwa kuwa imepata mbinu za ushindi ndani ya uwanja.Mchezo wake uliopita ilishinda jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Gwambina FC mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Biashara United ya Mara.Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa ushindi ambao wameupata ni salamu...
MWADUI FC MAJANGA, YAWEKA REKODI YAKE BONGO
KIKOSI cha Mwadui FC kimekuwa kwenye majanga baada ya kuyeusha pointi sita mfululizo kwa kupokea vipigo vikubwavikubwa.Kikosi hicho kimeweka rekodi ya kukubali vipigo vikubwa mara mbili mfulizo ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.Kwenye mechi hizo mbili mfululizo ambapo benchi alikaa Khalid Adam ameshuhudia vijana wake wakikubali kuokota nyavuni mabao 11 jambo ambalo linampasua kichwa kwa sasa.Vijana...
PRINCE DUBE WA AZAM MAMBO NI MAGUMU, DAKIKA 270
PRINCE Dube mtupiaji namba moja ndani ya Bongo akiwa na mabao sita kwenye Ligi Kuu Bara na pasi nne za mabao mambo yamekuwa magumu kwa sasa ndani ya kikosi hicho baada ya kasi yake ya kucheka na nyavu kuzima ghafla.Dube amehusika kwenye mabao 10 kati ya 15 ambayo yamefungwa na timu yake ya Azam FC, kibindoni ana tuzo ya...