VITA YA UFUNGAJI BORA MAMBO NI MOTO, AZAM YAPACHIKA WAWILI,
KWENYE orodha ya wafungaji Bongo nyota wa timu ya Azam FC, Prince Dube ni kinara wa kutupia akiwa nayo mabao sita na ametoa jumla ya pasi nne za mwisho.Azam FC kwa sasa ikiwa imefunga mabao 14 yeye amehusika kwenye mabao 10 kwa kuwa amefunga mabao sita na kutoa pasi nne za mabao.Vita yake kwenye ufungaji ni dhidi ya mshambuliaji...
KOCHA YANGA: MUHIMU POINTI TATU MENGINE YATAFUATA
CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kikubwa ambacho anakihitaji kuona kutoka kwa wachezaji wake ni kupata ushindi utakaowafanya wasepe na pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.Mechi ya kwanza Kaze alikiongoza kikosi chake Oktoba 22 mbele ya Polisi Tanzania na alishinda bao 1-0 Uwanja wa Uhuru.Kwa sasa kikosi cha Yanga kitakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi...
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI
MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la Championi Jumamosi
KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI USIPANGE KUKOSA NAKALA YAKO
KESHO ndani ya gazeti la Championi Jumamosi usipange kukosa nakala yako
RATIBA YA SUPER U 20 ITAKAYOANZA KUFANYIKA KESHO HII HAPA
KESHO, Oktoba 24, kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi yataanza mashindano ya vijana chini ya miaka 20 kutoka vilabu 8.Mashindano hayo yatashirikisha timu 4 za ligi kuuAzam FCYangaKMCJKT TZNa zingine za akademi za mitaaniKeptenMgosiTwalipoMashindano haya yameandaliwa na taasisi ya Same Sports Youth Investment na yalikuwa yafanyike Uwanja wa Chuo cha Bandari lakini kutokana na lengo lake kuu ambalo ni...
YANGA YAANZA KUSUKA KIKOSI KAZI CHA KUIMALIZA SIMBA NOVEMBA 7
KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, anataka kukibadilisha kikosi chake hicho kabla ya kuwavaa wapinzani wao Simba, Novemba 7. Katika mkakati huo, viongozi wa Yanga wamependekeza kwa Kaze kuwa asafiri na wachezaji wake wote waende Kanda ya Ziwa kwa ajili ya mechi dhidi ya Biashara United na Gwambina ili amtathmini mchezaji mmoja mmoja kabla ya kupata kikosi kitakachoivaa Simba.Yanga jana...
JOTO LA DABI LIMEANZA KUPANDA, SIMBA YAIFANYIA USHUSHUSHU YANGA
HATIMAYE Klabu ya Simba imeanza kuichunguza Yanga kuanzia ilipopata kocha mpya Cedric Kaze.Yanga ambayo imejifungia Kigamboni jijini Dar es Salaam, imekuwa ikifanya mazoezi kwa siku mara mbili, asubuhi na jioni ndani ya ulinzi mkali. Hata hivyo, awali Simba hawakuwa na presha kubwa na Yanga kwa kuwa kikosi chao kilionekana kutokuwa imara sana lakini baada ya kumpata kocha mpya upepo umeonekana...
PRINCE DUBE NI HABARI NYINGINE NDANI YA LIGI KUU BARA
MASHABIKI wamelinganisha kasi aliyoanza nayo mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Meddie Kagere na hii aliyoanza nayo straika mpya wa Azam, Prince Dube msimu huu, na hapo ndipo Championi Ijumaa lilipoamua kuingia mzigoni kujua nani alianza kwa kasi zaidi. Katika mechi saba za kwanza msimu uliopita, Kagere, raia wa Rwanda, alihusika kwenye mabao tisa kati ya 12 ambayo...
MTIBWA SUGAR:TUTAFANYA VIZURI 2020/21
THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kwa sasa wanaamini watafanya vizuri licha ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Zubeir Katwila kubwaga manyanga na kuibukia Klabu ya Ihefu.Kwa sasa Mtibwa Sugar ipo chini ya Vincent Barnaba ambaye ni kocha msaidizi ndani ya Mtibwa Sugar na mchezo wake wa kwanza kukaa kwenye benchi la ufundi alishinda bao 1-0 dhidi...
SIMBA MAJANGA TUPU NYOTA WATANO KIKOSI CHA KWANZA OUT
KUUMIA kwa beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe jana Oktoba 22 kunafanya jumla ya wachezaji watano wa Simba kuwa majeruhi.Nyota mwingine ambaye ni majeruhi ni Chris Mugalu, raia wa Congo ambaye alipata maumivu ya nyonga muda mfupi kabla ya timu hiyo kuvaana na Tanzania Prisons.Wengine ambao ni majeruhi ni pamoja na Meddie Kagere na John Bocco ambao wote...