MEDDIE KAGERE HATIHATI KUIKOSA YANGA NOVEMBA 7
MTUPIAJI namba moja ndani ya Bongo kwa misimu miwili mfululizo akiwa amefunga jumla ya mabao 49 ambapo alifunga mabao 23 msimu wa 2018/19 na mabao 22 msimu wa 2019/20 na mabao manne msimu wa 2020/21 Meddie Kagere kuna hatihati akaukosa mchezo dhidi ya Yanga, Novemba 7 kutokana na kusumbuliwa na majeraha.Kagere ana zali la kuwafunga Yanga ambapo kwenye mabao...
KUMBE KIUNGO MPYA WA YANGA ALIWAGOMEA MWANZO
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Said Ntibazonkiza, amesema timu hiyo ilianza kumfuatilia miezi miwili hadi mitatu iliyopita kabla ya kufikia makubaliano ya kusaini mkataba huku akitamba ametua kwa kazi moja tu ya kusaidia timu kutwaa mataji. Ntibazonkiza alisajiliwa na Yanga Oktoba 12 kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akiwa mchezaji huru ambapo vijana hao wa Jangwani walimnasa baada ya...
RATIBA YA MECHI ZA LIGI KUU BARA LEO OKTOBA 19
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo Oktoba 19 kwa timu nne kushuka uwanjani kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.Ratiba ipo namna hii:-JKT Tanzania iliyo nafasi ya 16 na pointi nne itamenyana na Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 12 na pointi 5, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma saa 8:00 mchana.Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 13 na pointi tano itamenyana na...
POGBA BADO YUPOYUPO MANCHESTER UNITED
KOCHA Ole Gunnar Solskjaer amekanusha tetesi kuwa staa wake, Paul Pogba yupo njiani kujiunga na Real Madrid, baada ya mchezaji huyo kusema kuwa ana ndoto ya kuichezea timu hiyo. Pogba ambaye alisajiliwa na Manchester United kwa pauni 89m amekuwa akihusishwa kujiunga na Madrid ambayo inanolewa Mfaransa mwenzake, Zinedine Zidane.Pamoja na kuwa katika presha kubwa ya timu yake kutocheza vizuri, Solskjaer...
YANGA WABEBA IMANI KUBWA KWA KOCHA MPYA
KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema kuwa anaamini mbele ya kocha mpya wa timu hiyo, Cedric Kaze, kikosi chao kitafanya vizuri msimu huu kwa kupata ushindi katika michezo ya ligi kuu na michuano mingine. Oktoba 15 Kaze alisaini mkataba wa miaka miwili kuinoa Yanga na Oktoba 16, jana Jumamosi alianza kazi rasmi ya kuwanoa wachezaji wake wanaojiandaa na...
TFF YATOA TAMKO KUHUSU NAMNA INAVYOSHUGHULIKIA KESI
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limeonesha kusikitishwa na baadhi ya taarifa zinazosambaa mitandaoni juu ya namna taasisi hiyo inashughulikia kesi zinazowasilishwa kwake na vilabu mbalimbali.Aidha TFF itaendelea kusimamia haki kwa vile na taasisi inayoendeshwa kwa misingi na utawala bora, hivyo kama kuna upande hauridhishwi na uamuzi wa vyombo vya chini ya TFF, utaratibu ni kukata rufani ngazi ya juu...
ISHU YA KATWILA KUBWAGA MANYANGA MTIBWA SUGAR IPO HIVI
IMEELEZWA kuwa, Zuber Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amebwagwa manyanga kutokana na timu hiyo kuwa na matokeo ya kusuasua kwa msimu wa 2020/21.Katwila ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa timu hiyo na alikuwa nahodha kwa sasa hayupo na timu kambini Morogoro ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC, unaotarajiwa kuchezwa kesho Oktoba...
HOFU YATANDA DIJK KUKAA NJE MIEZI SABA
BEKI kisiki ndani ya kikosi cha Liverpool, Virgil Van Dijk, anaweza kukaa nje miezi saba hii ikimaniisha huenda akazikosa mechi zote zilizosalia msimu huu, baada ya jana kuchezewa rafu mbaya na mlinda mlango wa Everton Jordan Pickford.Rafu hiyo alichezwa kwenye mechi ya Ligi Kuu England , Uwanja wa Goodison Park wakati Liverpool ikilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2.Aidha Liverpool...
KOCHA YANGA KUANZA KUTESTI MITAMBO NA POLISI TANZANIA
KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze kibarua chake cha kwanza ndani ya ardhi ya Bongo ni Novemba 22, Uwanja wa Mkapa itakuwa dhidi ya Polisi Tanzania.Kaze ambaye amesaini dili la miaka miwili Oktoba 16 tayari ameshaanza kukinoa kikosi cha Yanga kwa ajili ya mechi za ligi ambazo zipo mbele yake.Yanga ikiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi tano...
PRINCE DUBE WA AZAM FC AUTIKISA UFALME WA MK 14
PRINCE Dube, nyota wa Klabu ya Azam FC ameonekana kuutikisa ufalme wa Meddie Kagere wa Simba baada ya kuhusika kwenye mabao nane ndani ya timu yake kati ya 12 huku Kagere akihusika kwenye mabao manne kati ya 14 kwa msimu wa 2020/21.Dube, raia wa Zimbabwe alianza kwa makeke mchezo wake wa kwanza dhidi ya Polisi Tanzania alipotengeneza pasi yake...