HAWA HAPA MASTAA WATANO WENYE MKWANJA MREFU AFRIKA
MUZIKI kama zilivyo biashara nyingine, unalipa. Kwa hapa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiye anayetajwa kuwa na utajiri mkubwa japo vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa wapo wasanii wenye uwezo kifedha zaidi yake lakini kimsingi Kibongobongo bado imekuwa ni vigumu sana kupata data halisi za utajiri, tofauti na mataifa ya wenzetu.Hii ndio Top Five ya wasanii wenye pesa zao Afrika kwa mujibu wa majarida mbalimbali yanayofanya...
NYOTA HUYU WA MARSEILLE NI BALAA KWA MIPASI YA MWISHO
DIMITRI Payet, staa anayekipiga ndani ya Klabu ya Marseille ni balaa kwenye kutengeneza pasi za mwisho. Tangu msimu wa 2007/08 Payet amekuwa noma ndani ya Ligue1 kutokana na rekodi zake za asisti. Winga huyu ndani ya Ligue 1 amezichezea klabu tofauti na kwa wakati tofauti na kutengeneza rekodi yake ya tofauti. Alianza Nantes, kisha Saint Etienne, Lille na sasa anakipiga katika klabu...
LIGI KUU BARA 2019/20 HATARINI KUFUTWA NI NDANI YA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA
MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la CHAMPIONI Ijumaa, nafasi ya kushinda ndinga ni yako sasa
TSHISHIMBI:NASUBIRI SIMU YA MABOSI NISAINI
PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa kwa sasa anasubiri simu ya mabosi wa Yanga ili amalizane nao kwenye suala la kumwaga wino.Tshishimbi mkataba wake ndani ya Yanga umebakisha miezi minne na kumekuwa na msuguano wa muda juu ya kusaini kwake ndani ya Yanga kwa kile ambacho amesema kuwa anatazama dau litakalokuwa mezani.Nyota huyo amesema:"Nimeongea na mabosi wa Yanga...
KOCHA MANCHESTER CITY AWAPA SOMO MASHABIKI NA WACHEZAJI KUHUSU CORONA
PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa ni lazima kwa wachezaji na mashabiki kufuata kanuni za afya ili kujilinda na Virusi vya Corona.Dunia nzima kwa sasa inapambana na maambukizi ya janga la Corona jambo ambalo limefanya ligi nyingi duniani kusimamishwa zikisubiri hali kuwa shwari.Guardiola mwenye miaka 49 timu yake ya City ni mabingwa watetezi amesema kuwa dunia...
JACKSON MAYANJA: MAMBO BADO HAYAJWA SHWARI KWA SASA
JACKSON Mayanja aliyekuwa Kocha Mkuu wa KMC kwa sasa anakipiga anakinoa kikosi cha KFC cha Uganda amesema kuwa hali bado haijawa shwari kutokana na Virusi vya Corona.Mayanja kwa mwezi Februari alitwaa tuzo ya Kocha Bora ambapo alisema kuwa ilitokana na juhudi za wachezaji wake baada ya kukiongoza kikosi hicho kutoka kwenye nafasi ya 16 hadi ya 11 kwenye msimamo wa...
BEKI POLISI TANZANIA: UONGOZI WA POLISI TANZANIA UNAFUATILIA KWELI
WILLIAM Lucian, ‘Gallas’ beki wa kuliwa wa Polisi Tanzania amesema kuwa uongozi wa Polisi Tanzania upo makini kwenye kufuatilia maendeleo ya wachezaji pamoja na kujali maslahi ya wachezaji.Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita ikiwa imecheza mechi 29 kibindoni ina pointi 45 huku ikifunga mabao 29 na safu ya ulinzi imeruhusu mabao 26, kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa ili...
BEKI WA LIVERPOOL KUTIMKIA ARSENAL
DEJAN Lovren mwenye miaka 30 beki anayekipiga ndani ya Liverpool huenda akasepa msimu ujao.Beki huyo amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza kilicho chini ya Jurgen Klopp.Inatajwa kuwa Arsenal, Spurs na West Ham zipo kwenye hesabu ya kuwania saini yake.Timu yake ikiwa imecheza mechi 29 amecheza mechi tisa pekee za Ligi Kuu England na ametoa pasi moja ya bao.
MANCHESTER UNITED SASA YAMGEUKIA JAMES MADDISSON
JAMES Maddisson kiungo anayekipiga ndani ya Leicester City saini yake imekuwa Lulu ghafla kwenye timu zinazoshiriki Ligi Kuu England.Nyota huyo mwenye miaka 23 anakipiga pia kwenye Timu ya Taifa ya England.Inaelezwa kuwa Manchester United imebadili gia angani ambapo awali ilikuwa inamtaka Jack Grealish nahodha wa Aston Villa mwenye miaka 24.United imeanza kuyeyusha mipango ya kuinasa saini ya nahodha huyo...
WASHIDI WA JISHINDIE GARI KUSEPA NA ZAWADI ZAO LEO
IMEZIDI kuwa tamu sasa promosheni namba moja Bongo ya Chomoka na Gari inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publisher wazalishaji wa magazeti ikiwa ni pamoja na Championi na SpotiXtra ambapo washindi watatu leo wanakabidhiwa zawadi zao.Ofisa Masoko wa Global Publisher, Anthony Adam amesema kuwa baada ya kucheza droo ya kwanza kwa mafanikio Machi 25 bado promosheni inaendelea na wasomaji wanapaswa...