KABLA YA JUNI 30 MRITHI WA NDAYIRAGIJE KUJULIKANA
UONGOZI wa KMC umesema kuwa kwa sasa unaendelea na mchakato wa kumtafuta Kocha Mkuu atakayebeba mikoba ya Etienne Ndayiragije aliyetimkia Azam FC.Akizungumza na Salehe Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa kwa sasa michakato inaendelea ambapo tayari wameshawafanyia usaili makocha wengi wakubwa."Tunafanya usaili kwa umakini ili kumpata kocha atakayebeba mikoba ya mwalimu wetu ambaye ameondoka ,hivyo hatutakurupuka kumpata...
KALA JEREMIAH AJIANDAA KUVUTA JIKO
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Kala Jeremiah amesema kuwa kwa sasa anapambana kujitoa kwenye dhambi moja ya kuzini kwa kujipatia jiko lake hivi karibuni.Kala Jeremiah kwenye ngoma yake ya 'Dear God' ambayo ilimtambulisha vema alisema kwamba "Nisamehe dhambi ya kuzini" hali iliyomfanya ajithmini."Kwa sasa nipo kwenye mpango wa kuoa ili niepukane na dhambi niliyoomba msamaha, pia nashukuru mashabiki...
KOCHA YANGA AMLILIA HERITIER MAKAMBO
KOCHA wa zamani wa timu ya Yanga, Azam FC na Singida United Hans Pluijm amesema kuwa itachukua muda mrefu kwa mbadala wa mshambuliaji wa Heritier Makambo kuvaa viatu vya mshambuliaji huyo ndani ya ligi.Pluijm amesema kuwa kwenye suala la washambuliaji ambao wamezoea mazingira ya ligi ghafla ni pamoja na Makambo ambaye amekuwa ni injini ya mabao ndani ya Yanga hivyo...
NYOTA HUYU SIMBA ATAJWA KUBEBA MIKOBA YA BOCCO KWENDA POLOKWANE
IMEELEZWA kuwa baada ya uongozi wa timu ya Polokwane FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini kufeli kuipata saini ya nahodha wa Simba, John Bocco, sasa wamegeuza kibao kwa kumtaka nyota mwingine akazibe nafasi ya Bocco.Habari zimeeleza kwamba baada ya Uongozi wa Polokwane kushindwa kuipata saini ya Bocco sasa wamezungumza na uongozi wa Simba ili kuipata saini ya Adam...
EXCLUSIVE: SIMBA YAMTANGAZA BENO KAKOLANYA
UONGOZI wa Simba leo umemtangaza aliyekuwa mlinda mlango wa Yanga Beno Kakolanya kujiunga na kikosi hicho msimu ujao kwa kumpa kandarasi ya miaka miwili. Kakolanya alivunja mkataba wake na Yanga kwa kudai stahiki zake hali iliyoSimba sasa inakuwa na magolikipa watatu ambao ni pamoja na Aishi Manula na Deogratius Munishi
SINGIDA UNITED YA MINZIRO YASAKA WACHEZAJI 10 KATI YA 500
UONGOZI wa Singida United umesema kuwa wamejitokeza wachezaji zaidi ya 500 kwa ajili ya kufanya majaribio kwenye kikosi hicho ambalo lilianza Juni 12 litakamilika Juni 16.Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United,Cales Katemana amesema kuwa wamepokea jumla ya wachezaji 500 ambao wanafanyiwa mchujo chini ya kocha Felix Minziro kuwapata wachezaji 10."Tanzania kuna vipaji vikubwa na wengi wanapambana...
MATOLA WA LIPULI AIBUKIA POLISI TANZANIA, ASAINI MWAKA MMOJA
SELEMAN Matola amepewa kandarasi ya kuinoa timu ya Polisi Tanzania iliyopanda Daraja msimu huu kushiriki Ligi Kuu Bara.Matola ambaye alikuwa kocha wa Lipuli ametambulishwa leo wa ajili ya kuanza kuinoa timu hiyo na atafanya kazi kwa kushirikiana na Ali Suleiman ambaye ndiye mkurugenzi wa benchi la ufundi.Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa huo ni mwanzo tu...
KUMEKUCHA NAMUNGO, WAGOMEA WACHEZAJI WA MAJARIBIO
UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa kwa sasa haufikirii kusajili wachezaji wa majaribio na badala yake wanafanya kazi kubwa kusajili wachezaji wenye uwezo wa kushindana.Akizungumza na Salehe Jembe, Ofisa Habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia amesema kuwa baada ya kikosi kupanda ligi kuu, hesabu kubwa ni kusuka kikosi cha ushindani na sio cha majaribio."unajua kwamba ushindani wa kwenye ligi...
NYOTA WA BARCELONA AISHANGAA STARS, AIPA NAFASI YA KUFANYA MAAJABU AFCON
NYOTA wa zamani wa timu ya Barcelona, Chelsea, Inter Milan na timu ya Taifa ya Senegal, Samuel Etoo ameishangaa kuskia Tanzania inashiriki michuano ya Afcon mara baada ya kupita miaka 39.Etoo amesema kuwa wakati anacheza na Senegal alipata bahati ya kucheza na kikosi hicho mara kadhaa lakini na aliona vipaji vingi kwa wachezaji wa Tanzania."Nimeshangazwa kuskia kwamba Tanzania inashiriki...