DJUMA WA SIMBA KUIBUKIA KMC
MASOUD Djuma kipenzi cha mashabiki anapewa nafasi ya kutua bongo akiwa kwenye dawati la ufundi wa timu ya Manispaa ya Kinodoni 'KMC' ambayo kwa sasa ni ya kimataifa ikishiriki kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza.Djuma alikuwa kocha msaidizi wa Simba alifungashiwa virago baada ya kutokuwa na maelewano na Kocha Mkuu, Patrick Aussems 'Uchebe'.Habari kutoka ndani ya KMC zimeeleza...
NYOTA WA MWADUI AIYEE AWAAMBIA YANGA WAPELEKE MKWANJA MREFU
NYOTA wa Mwadui FC, Salum Aiyee amesema kuwa anatazama timu yenye mkwanja mrefu ili asaini kwani ofa alizonazo mkononi kwa sasa ni nyingi.Akizungumza na Salehe Jembe, Aiyee amesema kuwa amekuwa akizungumza na viongozi wengi wa timu mbalimbali ambao wanahitaji saini yake hivyo kikubwa kwake ni maslahi kwanza."Mimi najua kwamba timu yangu iliyonitambulisha kwa mashabiki ni Mwadui ila kama ofa...
KAZI IMEANZA SIMBA WAJIBU MAPIGO YA YANGA, WAANZA NA BOCCO MIAKA MIWILI
UNAAMBIWA Uongozi wa Simba baada ya kuona watani zao wa jadi Yanga wao wameanza na kiungo fundi Papy Tshishimbi kumuongezea mkataba wao wameanza kujibu kwa kuanza na nahodha wa kikosi hicho John Bocco.Bocco ni miongoni mwa nyota wanne ambao wamejiunga na kikosi hicho wakitokea Azam FC akiwa pamoja na mlinda mlango Aishi Manula, beki kiraka Erasto Nyoni, Shomari Kapombe...
TUWAACHE MKUDE, AJIBU WAFANYE YAO, TUELEKEZE MACHO CAIRO
NA SALEH ALLYMJADALA umekuwa mkubwa sana kuhusiana na viungo wawili, mmoja ni Ibrahim Ajibu ambaye ameichezea Yanga msimu uliopita na Jonas Mkude wa Simba.Hawa wote ni vijana wa Kitanzania ambao tayari wamejitengenezea ajira kupitia mchezo wa mpira wa miguu.Ni jambo guri sana kumuunga mkono mwenzako unapoona amefanikiwa katika jambo fulani. Sisi sote ni Watanzania, lazima tuungane mkono kwa maana...
Wanaompinga Amunike, wamesahau sababu ya Yanga kuitwa Kandambili.
“…mwalimu wetu ni raia wa Nigeria, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, ameshinda vikombe vya Afcon lakini ni mchezaji wa zamani wa Barcelona na timu zingine kama Zamalek…”“…Kwa wale ambao mnaufahamu mpira hambabaishwi, ni jina kubwa kwenye ulimwengu huu wa mpira…”Hayo ndio maneno ya awali kabisa ya Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wa...
USAJILI SIMBA NI BALAA TUPU, JIONEE MWENYEWE
SIMBA imesisitiza kwamba watafanya usajili wa aina yake msimu huu lakini wachezaji wawili watakaowasajili ni mshtuko.Kikosi hicho kilichopo chini ya muwekezaji Mohammed Dewji ‘Mo’ kimetwaa ubingwa mara mbili mfululizo na sasa kinajiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika inayoanza mwezi Agosti.Katika usajili wao mpya, Simba wametamka kwamba hawataleta mchezaji yeyote kwa majaribio kwani wao wameshavuka levo hiyo. Haji Manara ambaye...
VIFAA 21 YANGA HADHARANI, MASTAA WANNE WA KIGENI OUT
YANGA wameamua kwamba mastaa wanne wa kigeni watakwenda na maji na kwenye usajili wao mpya watakuwa na nondo tisa mpya za kutoka nje ya nchi.Awali Kocha Mwinyi Zahera alitaka kusajili wachezaji sita tu wa kigeni ambao ni watu wa kazi watakaozama moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza lakini sasa ameamua kubadili gia ili kujiweka fiti kwa Ligi ya...
YANGA YAMPA MKATABA KIPA AKIWA MISRI
MABOSI wa Yanga baada ya kusikia kwamba Azam FC wanamnyemelea kipa Metacha Mnata, wameamua kumpa mkataba kipa huyo fasta akiwa Misri.Yanga wanapambana vya kutosha kuhakikisha wanampata Metacha baada ya kushindwa kukamilisha kwa wakati dili lake akiwa kwenye kambi ya Taifa Stars jijini Dar es Salaam. Wakati Yanga wakiwa kwenye harakati hizo za kumchukua Metacha, Azam FC nao wamefuata kipa...
FOWADI MPYA YANGA USIPIME
HUYO Makambo wenu mtamsahau! Ndivyo unaweza kusema kufuatia fowadi mpya ya Yanga kuonekana ni moto na hii ni kutokana na takwimu zake za kutupia mabao.Yanga msimu uliopita ilimtegemea zaidi Heritier Makambo raia wa DR Congo ambaye akiwa Jangwani aliwajaza wapinzani kwa kufunga mabao 17 kwenye ligi kuu na sasa amewapa mkono wa kwaheri kuelekea Horoya AC ya Guinea.Baada ya...