KUHUSU USAJILI MPYA SIMBA…MBRAZILI ATAJA MASTAA ANAOWATAKA…AWAGUSIA KIBU NA BANDA…
Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameweka wazi mpango wa kuisuka timu hiyo katika usajili wa dirisha kubwa ili iwe bora kwenye msimu ujao kwenye mashindano wanayoshiriki. Simba SC kwa msimu wa pili mfululizo imemaliza bila kuwa na taji lolote, jambo ambalo linamlazimu kocha huyo kuhakikisha anakuwa na kikosi kipana ambacho kitahimili kucheza mashindano tofauti kwa mafanikio. Robertinho amesema...
MANULA, KAPOMBE WAIBUA JAMBO AZAM FC…MABOSI WAANZA ‘KUCHANGA KARATA UPYA”…
Uongozi wa Azam FC umesema kuwa hautakubali kufanya makosa ya kuwaachia mastaa wao kuondoka bure mwishoni mwa msimu huu na badala yake haraka watafanya maboresho ya mikataba kabla ya kumalizika mwishoni mwa msimu huu kwa baadhi ya wachezaji akiwemo Prince Dube na James Akaminko. Hiyo ni katika kuelekea dirisha kubwa la usajili kufunguliwa kwa ajili ya msimu ujao, Azam FC...
MASHUSHU WA CAF WAVAMIA HOTEL YA YANGA…WATOA ‘DATA’ ZA WASAZUI NA TAHADHARI…
Wakati wachezaji wa Yanga wakimalizia kula chakula cha mchana katika hoteli waliyofikia hapa Rustenburg, Afrika Kusini na viongozi wengine wakiendelea na shughuli za kitimu, ghafla waliingia Maofisa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ambao hawakutoa taarifa kabla. Viongozi hao walikuwa watatu mmoja akiwa amevalia fulana yenye nembo ya CAF na wengine nguo za kawaida na kuingia moja kwa moja hotelini. Walipoingia...
MAGAZETI SAUZI YAUZA NA STORI ZA YANGA TU….TIMU WENYEJI WAPEWA ‘ODDS’ NDOGO…
Baadhi ya magazeti ya hapa Afrika Kusini kwenye kurasa za michezo yameandika kuhusu Yanga kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC siku chache kabla ya mechi ya marudiano dhidi ya Marumo Gallants hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Tofauti ya timu hizi mbili ipo hivi, Marumo Gallants inapigana kujinusuru isishuke daraja kwenye Ligi yake wakati Yanga...
HUU HAPA MKAKATI WA BILIONEA WA YANGA KUHUSU NDOO YA AFRIKA…KAZI INAANZA LEO RASMI…
Baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa maboa 2-0 dhidi ya Marumo Gallants na kuweka mguu mmoja ndani ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Bilionea wa Yanga, Ghalib Said Mohammed ‘GSM’, amesisitiza kuwa anataka kuona kikosi hicho kikishinda ubingwa wa mashindano hayo. GSM ambaye Jumatano iliyopita alihudhuria uwanjani pamoja na familia yake na kushuhudia Yanga wakiibuka na ushindi wa...
MMOJA KATI YA HAWA KUTUA YANGA ….ENG HERSI APANIA KUFANYA ‘BALAH LA KIMADRID’ BONGO..
Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. hersi Said amesema kuwa msimu ujao watamsajili mshambuliaji kinara wa Ligi ya Afrika Kusini (PSL) ili kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya michuano ya ya ndani na Kimataifa. Hersi amesema hayo wakati akihojiwa na mwandishi nguli wa habari nchini Afrika Kusini jana. "Nitahakikisha ninampata mchezaji mmoja wa Afrika Kusini, hii sio kwa sababu ya mashabiki...
MUDATHIR AAIKA ISHU YA ‘KUTONGOZWA’ NA NABI…AFUNGUKA JAMBO LA MAYELE NA AZAM…
Kiungo wa mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara, Mudathir Yahya amesema kuwa mara tu baada ya kuachana na mabosi wake wa awali, Wauza Ukwaju wa Dar, Azam FC, Kocha Mkuu wa Wanajangwani, Nasreddine Nabi alimpigia simu kumhitaji ajiunge na kikosi chake. Mudathir amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari baada ya kuisaidia timu yake hiyo kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu...
KUHUSU ISHU YA KUSEPA ZAKE MSIMBAZI…KAPOMBE AVUNJA UKIMYA….AANIKA MSIMAMO WAKE..
Uongozi wa Klabu ya Simba SC umeanza kuboresha mikataba ya wachezaji wao inayotamatika mwishoni mwa msimu huu kabla ya kuanza kushusha vifaa vipya, kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa. Hii ni baada ya msimu huu tena kutoambulia taji lolote huku wakishindwa kufikia lengo lao la kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa...
HUJACHELEWA BADO….KWENYE USIKU WA ULAYA LEO..TEMBEA NA ODDS HIZI ZA MERIDIANBET…
Mbio sakafuni huishia ukingoni, hatimaye safari ndefu ya kumtafuta bingwa mpya wa Ligi ya Mabingwa na Uropa Ligi inaelekea ukingoni. Odds kubwa unazipata Meridianbet pekee machaguo kibao huku ukibashiri mubashara mechi zote wiki hii. Usiku wa mabingwa Ulaya unaenda kuweka historia kwa mara nyingine tena, katika dimba la Giuseppe Meazza itawakutanisha mahasimu wawili kwenye soka la Italia, Inter Milan vs...
KUELEKEA MECHI YA KESHO…WASAUZI WAJIKUTA NJIA PANDA…YANGA WASHINDWE WENYEWE TU…
Marumo Gallants ipo kwenye mtego unaohitaji mbinu na akili nyingi sana kuutegua ili wafanikiwe. Marumo ina mechi mbili (2) muhimu za maamuzi! Jumatano Mei 17, 2023 watacheza mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga ambapo tayari wako nyuma kwa mabao 2-0. Siku tatu baadae, Jumamosi ya Mei 20, 2023 watakuwa mzigoni kwenye mchezo wa...