KARIA: LIGI BONGO HATASIMAMA KISA KOMBE LA DUNIA…KUNA TIMU IKIFUNGWA NATUKANWA MIMI….
Kilio cha kuchezwa mfululizo Ligi Kuu ya Tanzania kimemfikia Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia ambaye amejibu mapigo kuwa imefikia hatua baadhi ya watu wanamtishia kuwa watamshtaki Shirikisho la Kimataifa (FIFA) ili afungiwe. Licha ya hayo, Rais Karia amesisitiza kuwa Ligi hiyo haitasimama hata katika kipindi cha michuano ya Kombe la Dunia kwani inapotokea viporo yeye ndiye...
KUELEKEA DIRISHA DOGO…KISINDA ‘OUT’ MBRAZILI WA SINGIDA ‘IN’…ISHU NZIMA IKO HIVI..
Yanga inaona bado inakosa huduma ya winga wa kisasa anayejua kutengeneza mashambulizi makali wakati wakisubiri ratiba ya kujua wataangukia kundi lipi katika hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini kuna mtu wanampigia hesabu ndefu. Yanga bado wanapiga hesabu waingie vipi Singida Big Stars kupata saini ya winga wa Kibrazil Dario Frederico ambaye amendelea kuwa na mwanzo mzuri katika...
TETESI:BAKHRESA KUPELEKA MAUMIVU YANGA….FEI TOTO NI SUALA LA MUDA TU KUTUA AZAM FC..
Ikiwa imesalia takribani miezi miwili dirisha Dogo la usajili la mwezi Januari kufunguliwa, inasemekana Bosi wa Azam FC, Yusuf Bakhresa ameanza kufanya michakato ya kuboresha kikosi cha Azam na rada yake imetua kwa Nyota wa Yanga SC, Feisal Salum (Fei Toto). Inasemekana Fei Toto na Bakhresa wapo mezani kujadili matakwa ya mchezaji huyo na endapo wataafikiana basi kiungo huyo aliyejizolea...
MATOLA AKIRI KUSEPA SIMBA…JUMA KASEJA KURUDI KUNDINI…KOCHA WA VIUNGO HUYU HAPA…
Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amethibitishia kwamba anaondoka kwenye benchi la ufundi la timu hiyo kwa muda akapige shule kidogo. Matola ambaye ni nahodha wa zamani wa Simba na Taifa Stars, amepata fursa ya kwenda kusoma kozi ya leseni A ya CAF, ataanza Novemba 21 ambapo atasoma kwa wiki mbili, kisha atarejea kikosini hapo kwa kuyafanyia kazi kwa vitendo...
KISA SIMBA NA YANGA…WADHAMINI LIGI KUU WAIBUKA NA HOJA MPYA…WAWEKA WAZI VIAUMBELE VYAO…
Mkurugenzi wa fedha na utawala wa NBC ambao ni wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Waziri Barnabas amesema imefika wakati wa kuifanya dabi ya Kariakoo kuwa na thamani zaidi ya kutazama tu dakika 90. Amesema dabi ya Kariakoo inavutia maelfu ya mashabiki duniani hivyo haipaswi kuishia ndani ya dakika 90 za uwanjani bali Shirikisho (TFF) na klabu husika zitengeneze utaratibu...
BAADA YA KUIPAISHA SIMBA KIMATAIFA…GOMES AFANYA KWELI …AWAPA UBINGWA WAAABU…
Kocha wa zamani wa Klabu ya Simba SC, Didier Gomez ameiwezesha Klabu yake ya sasa ya Al-Wehdat SC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Jordan kutwaa Ubingwa wa Kombe la Jordan Cup Baada ya kuibuka na ushindi wa Goli 1-0 dhidi ya Al-Aqaba SC. Fainali ya Kombe hilo imemalizika mda mfupi uliopita ambapo Gomez ameiwezesha Klabu hiyo kushinda Ubingwa wa 11 wa...
BENZEMA: RONALDO ‘KANILIA BUYU’ TOKA NISHINDE TUZO YA BALLON d’Or …
Mshambuliaji wa Real Madri, Karim Benzema amekiri kuwa mchezaji mwenzake wa zamani kikosini hapo, Cristiano Ronaldo hajampongeza kwa kushinda Tuzo ya Ballon d'Or aliyonyakua Oktoba mwaka huu licha ya urafiki mkubwa walio nao. Ronaldo raia wa Ureno ambaye kwa sasa anaitumikia Man United, ameshashinda mataji mengi ikiwemo Ballon d'Or tano ambapo Benzema alishinda Tuzo hiyo hivi karinbuni katika ardhi ya...
EHEE…MASTAA BONGO WAMVULIA KOFIA ‘BABU KAJU’…KAPOMBE KASHINDWA KUJIZUIA KAFUNGUKA HAYA…
Ubora ulioonyeshwa na kiungo wa Yanga, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ katika mechi yao ya marudiano ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain, umewaibua mastaa mbalimbali wanaocheza Ligi Kuu Bara huku viungo wa Yanga wakimpigia saluti. Sure Boy alianza kwenye mchezo huo na Yanga ilishinda bao 1-0 na kuonyesha uhai eneo la kiungo...
INJINIA HERSI USO KWA USO NA MANGUNGU….WADAU WAPISHA WAKAE WENYEWE…
Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said na Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu ni miongoni mwa watu ambao wamehudhuria mkutano mkuu wa 17 wa Kawiada wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unaofanyika leo Novemba 14 jijini Mwanza. Viongozi hao wamekaa meza moja wakifuatana, ambapo Mangungu alifika mapema na kukaribishwa kwenye meza hiyo ambayo pia wamekaa viongozi wa KMC na Azam huku...
HUYU NI MFALME WA MERIDIAN USSD BETI NA KITOCHI…ASHINDA MAMILIONI KIRAHISII…
Haijalishi unatoka familia gani ili uwe Mfalme, Yeyote aliyepo kwenye famila ya Meridianbet ni mfalme wa Maisha yake, na Leo Meridianbet wanamleta kwenu Mfalme wa Beti na Kitochi kwa USSD. Mfalme huyu anaitwa Zamiru Mohammed kutoka Chalinze, Gwiji aliyejishindia Pesa Taslimu TZS 1,324,878/= Milioni moja, Laki tatu na Elfu Ishirini na nne, Mia nane sabini na nane, alibeti kwa dau...