BAADA YA KUWAONA MOTO WA YANGA JUZI…AHMED ALLY KAGUNA KISHA AKASEMA SIMBA HAIFUNGWI NG’OO…
Yakiwa yamesalia masaa machache kabla ya mchezo wa Simba na Ihefu pale kwa Mkapa Dar, uongozi wa klabu ya Simba umefunguka kuwa timu hiyo haitafungwa tena msimu huu. Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahemd Ally alisema, timu ambayo inakuwa inawania ubingwa haiwezi kuwa na matokeo ya kupanda na kushuka, kwa maana ya kufungwa, kushinda na kutoka sare, badala...
BAADA YA KUIPELEKA YANGA MAKUNDI…AZIZ KI AKIMBILIA KWAO ‘KUJICHAJISHA NGUVU MPYA’…
Mfungaji wa bao lililowavusha Yanga kwenye hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, Stephen Aziz Ki hajarudi na wenzake kwa ruhusa maalum ya uongozi. Nyota huyo amepewa ruhusa ya kwenda kwao Ivory Coast baada ya kufungiwa michezo mitatu ya ligi. Yanga wametua mchana huu kutoka Tunisia kupitia Dubai na wanatarajia kwenda Mwanza leo saa moja usiku tayari kwa mchezo wa Jumapili...
MPOLE: GEITA WANANIONEA…MBONA WENGINE HAWAKO NA TIMU NA WANALIPWA MSHAHARA…
Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, George Mpole, ameibuka na kufunguka mengi makubwa yanayomuhusu mara baada ya kutoonekana kwa muda kikosini hapo. Hiyo ikiwa siku ni siku chache zimepita tangu uongozi utoe taarifa za mshambuliaji huyo kutoweka kambini wakati timu hiyo ikiendelea kucheza michezo ya Ligi Kuu Bara. Mpole alisema hayupo katika timu hiyo, kutokana na kuuguza majeraha ambayo...
BAADA YA KUFUZU MAKUNDI CAF…BEKI YANGA ‘ALAMBA MCHANGA’ KULETA MAKUBWA ZAIDI…
Beki wa kati wa Yanga Dickson Job amefunguka kuwa kwa kuwa wamefanikiwa kutinga kutinga kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, watafanya makubwa na watakwenda mbali zaidi na kufanya makubwa. Job alisema kuwa anajua mashabiki wa Yanga walikuwa wanahitaji kuona timu yao inafika kwenye hatua ambayo imefika kama ambavyo wachezaji na benchi la ufundi walikuwa wanatamani pia, lakini...
MAYELE: TUMEFUZU KWA SABABU YA MATUSI YA MASHABIKI…WALITUPA HASIRA..
Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ameweka wazi kuwa kulikuwa na sababu nyingi sana ambazo zilipelekea wao kupambana na kupata bao la ugenini na la ushindi wakiwa Tunisia na kuwatoa Club Africain. Mayele alifunguka kuwa moja ya kitu ambacho wao kama wachezaji kilikuwa kinawaumiza ni maneno ya kejeli kutoka kwa mashabiki ambao walikuwa wanasema hawana faida kwenye timu hiyo kwa kuwa...
MERIDIANBET YAWASHIKA MKONO HOSPITALI YA TUMBI…
Kampuni ya Meridianbet iliyoambatana na timu nzima ya masoko, akiwemo meneja masoko wa kampuni hiyo Ndugu Matina Nkurlu, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Maudhui Bw Twaha Ibrahimu, leo Novemba 11, 2022 ilitembelea Hospital ya Rufaa ya Tumbi mkoa wa Pwani, kwaajili ya kutoa msaada wa vifaa kwa matumizi ya wagonjwa katika hospitali hiyo. Katika kuunga mkono juhudi za Serikali...
AJIBU AMLIZA ASUKILE…AMSHANGAA KUONA ANAVYOPOTEA KILA SIKU…
Nahodha wa Prisons, Benjamin Asukile ameshangazwa kuona kipaji cha kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Ibrahim Ajibu kinapotea wakati angeweza kukipambania, akiamini hakuna timu ambayo ingeacha kumchukua nje ya nchi. Asukile alichambua aina ya uchezaji wa Ajibu namna anavyoona nafasi za kufunga akiwa ndani na nje ya 18 na sio hilo tu bali na uwezo wake wa kuchezesha timu mbele na...
BAADA YA KUWAGOMEA…GEITA WAAMUA KUMALIZANA MAZIMA NA NTIBAZONKIZA…
Viongozi wa Geita Gold wamemalizana na kiungo wake mshambuliaji, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ baada ya kutoweka kambini na hata mastaa wengine waliokuwa hawapo wamerejea. Mbali na Saido mastaa wengine waliotimka kambini kutokana na madai mbalimbali ni Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Hussein Bakari, Samson Sebusebu na Oscar Masai. Lakini wameshayajenga na viongozi kimyakimya na wamerejea isipokuwa George Mpole. Saido, nyota wa zamani wa Yanga...
LAANA YA KUMUACHA KISINDA NA CHAMA YAWATAFUNA BERKANE…WATEMESHWA UBINGWA WA CAF…
RS Berkane wameondoshwa kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho na klabu ya Tunisia US Monastir kwa Agg ya bao 1-0. Berkane ndiye bingwa mtetezi wa #CAFCC msimu uliopita wakitwaa kwa jumla ya Penati 5-4 dhidi ya Orlando Pirates. Mchezo wa jana wa raundi ya pili umemalizika kwa sare ya 0-0 huku wakipoteza wa mwanzo kwa bao 1-0 na kushindwa kufuzu hatua...
BAADA YA KUPATA SARE YA KIBAHATI BAHATI JUZI…MGUNDA APANGA ‘KUISHINDILIA’ IHEFU KESHO…
Baada ya sare ya bao 1-1 waliyoipata kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Singida Big Stars, Kocha wa Simba, Juma Mgunda ameweka wazi kuwa mechi yao ijayo dhidi ya Ihefu FC itakuwa ni ya kurekebisha makosa ya mechi iliyopita. Kesho Jumamosi Simba watashuka dimbani kucheza na Ihefu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar. Mgunda alisema kuna kila sababu ya wao kupata ushindi...