MAMBO SABA YAMTOA ZORAN SIMBA…BOKO, ONYANGO WATAJWA…KISINDA KUITIKISA TFF IJUMAA…
Pitia ukurasa wa mbele wa gazeti la MwanaSpoti la leo Jumatano.
KUELEKEA MECHI YA KESHO ….SHIDA KWA ONYANGO BADO IKO PALE PALE…JAMBO LAKE NA SIMBA KUMBE BADO SANA…
Beki kisiki wa Simba SC, Joash Onyango kesho hatakuwa sehemu ya kikos pindi Wekundu hao watakapovaana na KMC kesho Septemba 7, 2022.Kwa mujibu wa msemaji wa Simba, Ahmed Ally, Onyango hakufanya mazoezi na timu kwa siku kadhaa hivyo hatoweza kucheza na kwamba kuna masuala yake anamalizana na klabu ndipo hatma yake itangazwe.“Onyango hajafanya mazoezi na wenzake hivyo hatakuwepo kesho...
KUHUSU KOCHA ATAKAYERITHI MIKOBA YA MAKI…SIMBA WATOA TAMKO RASMI…WATAJA TAREHE YA KUMTANGAZA…
Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally amesema, baada ya kuachana na aliyekuwa kocha Mkuu Zoran Maki, mchakato wa kumpata mrithi wake umeanza haraka na wanatarajia kuwa naye kabla ya mechi yao ya Kimataifa dhidi ya Nyasa Big Bullet ya Malawi.Ahmed amesema, kwenye orodha ya makocha ambao waliomba wakati wanatafuta kocha kabla ya msimu huu kuanza, walikuwepo makocha wengine wawili...
BAADA YA MAKI KUONDOKA ….SIMBA WAANIKA MUSTAKABALI WA ‘STRAIKA MZUNGU’…WADAI HALIPO KWENYE MAKUBALIANO…
Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally amesema straika Mzungu, Dejan ataendelea kuwepo klabuni hapo kwani hahusiani moja kwa moja na kocha Zoran Maki aliyefungashiwa virago mchana huu.Akizungumza mara baada ya kufanya mkutano wa ajili ya mechi yao kesho dhidi ya KMC, Ahmed alisema, wamefikia makubaliano ya kuachana na kocha Mkuu pamoja na kocha wa viungo Sbai Karim na kocha...
FT:YANGA 2-2 AZAM FC….’FEI TOTO’ AFANYA MAAJABU YA DUNIA…MAYELE AFANYIWA ‘UNDAVA’…MORRISON MHHH…
MABINGWA watetezi Yanga wametoka nyuma na kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Matajiri wa Chamazi Complex Azam FC mchezo wa ligi Kuu ya NBC uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.Shujaa wa Yanga ni Feisal Salum (Fei Toto) aliyetokea benchi na kwenda kufunga mabao yote mawaili dakika ya 56 na 77.Azam FC walikuwa wa kwanza...
GEITA GOLD WAKUTANA NA YA YANGA KWA SAIDO NTIBANZONKIZA…TFF WAONDOA JINA LAKE KWENYE MAJINA YA CAF….
Nyota wa Geita, Mrundi Saido Ntibazonkiza ambaye amesaini mkataba na timu hiyo akitokea Yanga jina lake halijaonekana kwenye wachezaji wa timu hiyo wanaoiwakirisha kimataifa.Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa orodha ya wachezaji 40 ambao watashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika huku jina la Saido halimo katika orodha hiyo.Akizungumza suala hilo Katibu wa timu hiyo Simon Shija amesema:"Mpaka sasa...
SAKATA LA KISINDA…YANGA NA TFF NI JINO KWA JINO…MABOSI JANGWANI WAIVIZIA TAARIFA YA KAMATI KUAMSHA MOTO…
Inaelezwa kuwa Uongozi wa Klabu ya Yanga SC umepanga kupeleka malamiko kwenye kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kugomea uamuzi wa TFF wa kuzuia Usajili wa Kisinda, huku wakiona kuna hujuma zinasukwa kupunguza makali ya timu yao.Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Simon Patrick amesema; "Tulimsajili Tuisila Kusinda ndani ya muda, shirikisho la soka Tanzania (TFF) likatusaidia kupata (ITC)...
DAKIKA KADHAA KABLA YA MECHI NA YANGA KUANZA….SOPU AJIAPIZA KUMFANYA MWANYETO ATELEZE TENA LEO…
Mshambuliaji mwiba kwa mabeki wa Yanga, Abdul Seleman 'Sopu' amesema anatamani kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoivaa Yanga jumanne baada ya kutamba kuwa fiti kwa asilimia 100 huku akitamba ametumia mchezo dhidi ya Uganda kuimarisha mwili wake. Sopu aliye weka rekodi ya kumfunga mabao 3-0 kipa wa Yanga Djigui Diarra kwenye mchezo wa fainali kombe la shirikisho la Azam (FA) atakutana...
KUELEKEA MECHI NA SIMBA….HITIMANA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA KUCHOSHWA NA UTUMWA WA TIMU KUBWA…
Kocha Mkuu wa KMC, Thierry Hitimana amesema ni muda sahihi kwake wa kukata minyororo ya unyonge kwa kutaka kuvunja uteja uliotawala kwa timu yake dhidi ya Simba wakati zitakapovaana kesho kwenye mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara.Timu hizo zinakutana kwenye mechi ya kwanza msimu huu ikiwa ni mchezo wa tatu wa kila mmoja tangu Ligi Kuu ilipoanza Agosti...
BAADA YA KUACHANA NA SIMBA…WAARABU WAMPA DILI LA ‘CHAP CHAP’ ZORAN MAKI…MSHAHARA WAKE MPYA BALAA TUPU…
Klabu ya Al Ittihad Alexandria ya ligi kuu nchini Misri, imemtangaza Mserbia Zoran Maki (60) kuwa kocha wao mkuu mpya zikiwa zimepita saa kadhaa kocha huyo kutangazwa kuachana na Simba SC aliojiunga nao mwezi Julai mwaka huu.Zoran ambaye ni raia wa Serbia amondoka Simba na wasaidizi wake akiwemo kocha wa makipa na kocha wa viungo, amesaini mkataba wa miaka...