Home Uncategorized DAH! MWANA TAMBWE KUMBE AMEWEKWA KIPORO….

DAH! MWANA TAMBWE KUMBE AMEWEKWA KIPORO….




Huku Yanga ikimuweka kiporo mshambuliaji wake, Amissi Tambwe, nyota huyo amepata ofa moja kutoka nje ambayo hajaiweka wazi.

Tambwe ni mmoja kati ya wachezaji wa Yanga ambao wamemaliza mikataba yao ndani ya klabu hiyo na mpaka sasa haijafahamika kama ataendelea kuwa hapo au la.

Straika huyo amekuwa na Yanga kwa msimu zaidi ya mitatu na amefanikiwa kutwaa mataji matatu kikosini hapo huku akiibuka mfungaji bora msimu wa 2015/16 kwa kufunga mabao 21.

Awali alikuwa akiitumikia Simba msimu wa 2013/14, ambapo katika msimu huo alifunga mabao 19 na kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara.

“Ni kweli mkataba wangu na Yanga umeisha, uongozi umepanga kuzungumza baadaye, lakini kuna timu ambazo  zinahitaji kufanya mazungumzo na mimi, ni za hapa Tanzania na moja ni ya nje.

“Ninaamini bado nina uwezo wa kupambana popote pale nitakapokwenda iwe hapa Bongo na hata huko nje,” alisema Tambwe.

SOURCE: CHAMPIONI

SOMA NA HII  KOCHA HUYU ALIYEMNYOOSHA MBELGIJI WA YANGA ANAWINDWA ATUE JANGWANI