UONGOZI wa Kagera Sugar itakayocheza Play off na Pamba, umesema kuwa hakuna tatizo kwa wachezaji wao kujiunga na vikosi vingine msimu ujao kwani maisha ya soka ni changamoto kila siku.
Nyota wa Kagera Sugar kama mshambuliaji Kassim Khami, Ramadhan Kapera wamekuwa wakitajwa kusepa msimu ujao kujiunga na timu nyingine mpya ikiwa ni pamoja na Simba, Yanga na Azam FC.
Akizungumza na Saleh Jembe, kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa maisha ya mchezaji si ya kudumu sehemu moja hivyo kama kuna timu inahitaji saini za wachezaji ifuate utaratibu.
“Maisha ya mchezaji si ya kudumu sehemu moja inategemea na mahitaji hivyo utaratibu upo wazi na kwa atakayekamilisha ni ruksa kujiunga timu anayoipenda,” amesema.