Home Uncategorized MEDDIE KAGERE AFICHUA SIRI YA MAFANIKIO

MEDDIE KAGERE AFICHUA SIRI YA MAFANIKIO


NYOTA wa Simba, Meddie Kagere amesema kuwa kikubwa kinachompa mafanikio kwenye soka ni kujikubali yeye mwenyewe na kujipa changamoto yeye mwenyewe.

Kagere ni mfungaji bora wa msimu huu kwenye ligi kuu akiwa ametupia jumla ya mabao 23 ana tuzo mbili mkononi ya mfungaji bora wa mwaka na mchezaji bora wa mwaka ndani ya klabu ya Simba aliyopewa kwenye tuzo za Mo.

“Najikubali mwenyewe na kujipa changamoto mimi mwenyewe, siangalii wengine wamefanya nini ama wanasema nini kikubwa napambana kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu,” amesema Kagere.

SOMA NA HII  AZAM FC: TUNA KAZI NGUMU YA KUFANYA