habari za SIMBA NA YANGA
Habari za michezo

KWENYE DABI SIMBA ANAINGIA KAMA TIMU YA PILI

Abubakar October 14, 2024 10:16 am

Kuelekea mchezo mkali wa Dabi ya Kariakoo, Oktoba 19 tayari mambo yamezidi kupamba moto, ambapo joto kali limezidi kupanda kwa kasi kwenye kambi za Simba na Yanga.

Wakati hiyo yanaendelea, nao wachambuzi na wadau mbalimbali wa Soka wameendelea kutoa maoni na mitazamo yao juu ya mchezo huo.

“Tunakubaliana kuwa Simba Sc inajengwa na kocha Fadlu Davids anaendelea kukijenga kikosi bora hivyo bado naamini hata kwenye mchezo ujao wa dabi dhidi ya Yanga ambao Simba ndio mwenyeji ila bdao wanaingia kama timu ya pili”

“Japo kwenye dabi lolote linaweza kutokea ila Yanga anaingia kama timu bora kutokana na matokeo ya hivi karibuni kati ya hizo timu mbili walipokutana kwenye dabi” Ashraf Mchambuzi.

MSHERY NA ALLY SALIM WANATEGEMEWA NA TAIFA. WANANCHI NJOONI HUKU KUNA UJUMBE WENU OKTOBA 19 MNAENDA KUKAANGWA