Habari za Simba, Ahmed Ally
Habari za Simba Leo

WANANCHI NJOONI HUKU KUNA UJUMBE WENU OKTOBA 19 MNAENDA KUKAANGWA

Abubakar October 14, 2024 10:26 am

Semaji la Simba Sc Ahmed Ally, anasema siku ya Tarehe 19 Oktoba katika Dimba la Benjamin Mkapa Wananchi wanaenda kukaangwa kwenye mchezo wa Derby ya Kariokoo hivyo wana lunyasi wajitokeze kwa wingi siku hiyo.

Ahmed ameyasema hayo akiwa Tabata Kimanga Jijini Dar Es Salaam baada ya uzinduzi wa Tawi la Simba Sc lililozinduliwa jana.

“Tarehe 19 kuanzia majira ya saa 10 jioni tuna jambo letu Wanasimba, katika dimba la Mkapa tuna kazi ya kwenda kumkaanga mtu, tuna kazi ya kwenda kumkamua mtu tarehe 19, tuna kazi ya kwenda kumnyonyoa mtu na kumpelekea Ubaya Ubwela” Ahmed Ally

Katika mechi za hivi karibuni Yanga wamekua na takwimu nzuri wanapokutana na Simba, wakiwa na namba nzuri za ushindi ukiwemo ule ushindi wa mabao 1-5.

KWENYE DABI SIMBA ANAINGIA KAMA TIMU YA PILI HIVI NDIVYO ALI KAMWE NA AHMED ALLY WALIVYOTAMBIANA KUELEKEA DABI YA KARIAKOO.