Habari za Simba SC
Habari za michezo

MSHERY NA ALLY SALIM WANATEGEMEWA NA TAIFA.

Abubakar October 14, 2024 10:10 am

WALINDA Mlango wa Simba na Yanga Ally Salim Katolo na mwenzake AbdulTwalib Mshery wanategemewa sana na taifa, lakini nafasi zao za kucheza kwenye vilabu vyao ni finyu.

Hayo yamesemwa na Mchambuzi wa michezo nchini kupitia kituo cha redio cha Crown Fm, Magunga.

“Golikipa Abuutwalib Mshery ( Yanga Sc ) na Ally Salim (Simba sc ) wanategemewa zaidi kwenye mahitaji ya ndani ya timu ya Taifa lakini hawachezi mechi ya kutosha kwenye vilabu vyao na inawezekana wanashindwa kuondoka kutokana na ukata wa fedha uliopo ndani ya vilabu vingine ukilinganisha klabu walizopo kwa sasa”

“Mshery kwasasa Yanga Sc hapati namba sana kutokana na uwepo wa golikipa namba moja Diarra anafanya vizuri zaidi ila pia Ali Salim atumiki sana baada ya uwepo wa Moussa Camara”

ODDS KUBWA NA MACHAGUO ZAIDI YA 1000 YAPO MERIDIANBET… KWENYE DABI SIMBA ANAINGIA KAMA TIMU YA PILI