Jana kulikuwa na utoaji tunzo wa klabu za Simba, kitu ambacho ni kikubwa na chenye kuigwa kwa vilabu vingine ndani ya nchi yetu.
Kuna vitu vingi sana ambavyo vilionekana jana. Inawezekana mjadala mkubwa ni kwenye tunzo ambazo zimetolewa.
Lakini kwangu mimi kuna kitu kimoja ambacho nilikitazama jana. Uvaaji wa wachezaji na benchi la ufundi wa Simba.
Uliwatazama walivyokuwa wamevaa?. Walikuwa wamevaa suti maridadi sana. Suti ambazo ziliwakaa vizuri sana.
Suti ambazo ziliwapendezea sana, walikuwa wanatamanika sana kuwatazama jana. Hivo ndivyo ambavyo mchezaji anatakiwa kuvaa kwenye hafla kama hizo.
Jana wakati nawatazama nilikuwa najiuliza hawa ni wachezaji wa Manchester United au RealMadrid? Walikuwa wamependeza sana.
Kitu hiki ni kizuri sana kibiashara, picha ya bidhaa ya Simba inaonekana vizuri mbele ya macho ya wengi ikiwemo hata wafanyabiashara.
Kitu hiki huongeza thamani sana ndani ya bidhaa husika kwa sababu hutoa tafasri moja ambayo ni kubwa sana kibiashara kuwa Simba wamejipanga kwenye kila kitu.
Yani ndani ya timu kuna mpangilio mzuri kwenye kila idara, idara ya mavazi iliandaliwa kabisa kwa ajili ya kuwavalisha wachezaji na idara zingine ziliandaliwa kwa ajili ya kufanya kazi ipasavyo.
Mfanyabiashara huenda sehemu ambayo kuna mpangilio mzuri wa kila kitu. Pesa huenda sehemu ambayo kuna mpangilio, pesa haiendi sehemu ambayo hakuna mpangilio.
Wakati jana Simba walionekana kujipanga vizuri kuanzia kwenye idara ya mavazi, wenzao Yanga wao bado hawajafikia huku.
Unakumbuka ile hafla ya kufuturisha iliyifanyika wiki iliyopita pale Serena Hotel?. Unakumbuka wachezaji wa Yanga walivyokuwa wamevaa na benchi la ufundi walivyokuwa wamevaa?
Unaikumbuka picha ya pondamali na vazi lake ?. Kwa kifupi hakukuwepo na mpangilio mzuri wa mavazi kwa wachezaji na benchi nzima la ufundi.
Walivaa ovyo, kila mtu alivaa kivyake. Hivi ilishindikana kweli Yanga kutafuta mbunifu wa mavazi akawavalisha Yanga kanzu ?
Kukawa na mpangilio mzuri wa hafla?. Walichokifanya Yanga ni kuishusha thamani ya bidhaa ya Yanga.
Wanaikimbia dunia, wanaikwepa dunia na hawataki kuendana nayo kabisa hii dunia ya kibiashara.
Kumbuka nimekuambia pesa huenda sehemu ambayo kuna mpangilio mzuri. Kama Yanga watashindwa kujipangiliwa vizuri ni ngumu kupata watu wa kuja kuweka pesa ndani ya timu.
The post Yanga walivaa ovyo kwenye futari, Simba walifundisha kuvaa Yanga Jana. appeared first on Kandanda.