Home Uncategorized YANGA YAFUNGUKA JUU YA KUMSAJILI NDEMLA

YANGA YAFUNGUKA JUU YA KUMSAJILI NDEMLA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kumsajili kiungo wa Simba, Said Ndemla ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na kikosi chake.

Zahera amesema kuwa mpango wake ni kuwa na kikosi bora ambacho kitakuwa na ushindani msimu ujao kutokana na aina ya wachezaji ambao anawataka.

“Sina mpango wa kumsajili Said Ndemla, simjui huyo mchezaji na hayupo kabisa kwenye hesabu zangu.

“Nataka kufanya usajili ambao utakuwa na tija hivyo mashabiki wa Yanga watulie wasiwe na presha kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.

SOMA NA HII  MCHEZO WA KAGERA SUGAR V PAMBA WAINGIWA NA DOA, DAKIKA 16 ZAPITA