Home Uncategorized Kwa mujibu wa kanuni, Lipuli hawakustahili.

Kwa mujibu wa kanuni, Lipuli hawakustahili.

Kimsingi si Lipuli Fc ndio alitakiwa aende kushiriki michuano ya Kimataifa kwa msimu ujao kwa maana ya Kombe la shirikisho Africa na ni KMC kwa mujibu wa kanuni.

Baada ya CAF kuthibitisha Tanzania itakua na wawakilishi wanne katika michuano ya msimu ujao ya CAF, KMC alitangazwa kuwa ndiye atakewakilisha nchi katika Kombe la shirikisho akichukua nafasi ya mshindi wa tatu ambaye ndiye bingwa wa Kombe la FA linalojulikana Azam Sports Federation Cup.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano zilizofanyiwa marekebisho na Kamati ya Utendaji ya TFF , timu ya kwanza inayowakilisha Kombe la Shirikisho ni mshindi wa FA na timu ya pili ni mshindi wa tatu katika msimamo wa ligi kuu.

Kanuni inasema iwapo nafasi ya tatu imeshikwa na timu ambayo ni mshindi wa FA, timu iliyoshika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi ndiyo itakayochukua nafasi. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni na taarifa rasmi kutoka TFF baada ya kandanda kufuatilia.

Msimu wa 2018/2019

# Timu P GD Pts
1 Simba SCSimba SC 38 62 93
2 Yanga SC 38 29 86
3 Azam FC 38 33 75
4 KMC FC 38 15 55

Kwa maana hii, kama Lipuli Fc inadhani hii ilikuwa nafasi yake, basi hakukuwa na haja ya fainali ya ASFC.

Kandanda imeingia ndani zaidi ya Kanuni hiyo, iwapo mshindi wa FA atakuwa ni timu ambayo ipo nafasi ya kwanza au ya pili, nafasi ya Kombe la Shirikisho atapewa timu iliyocheza fainali ya FA kwasababu tayari bingwa huyo atakua anawakilisha Ligi ya Mabingwa Africa.

Kwa kesi hiyo kama Azam FC angemaliza akiwa bingwa wa Ligi Kuu basi Lipuli FC angechukua nafasi kucheza Kombe la Shirikisho.

Hii itazipa nidhamu ya ushindani kwa timu zote katika mashindano yote mawili.

The post Kwa mujibu wa kanuni, Lipuli hawakustahili. appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  VIDEO:CHEKI MATIZI YA CLATOUS CHAMA YALIVYO