Klabu ya Simba iko hatua za mwisho za kumsainisha mkataba mshambuliaji wa klabu ya Police FC ya Uganda, Juma Balinya mwenye umri wa miaka 27.
Balinya alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Uganda kwa sasa yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Uganda.
Taarifa zinasema kuwa tayari Simba wametuma mtu wao ambaye ameambatana na wakala wake Patrick Gakumba kwenda Abu dhabi.
Gakumba inaelezwa ameelezwa kila kitu juu ya kuhakikisha mchezaji huyo anatua Simba na dalili zikionesha anaweza akawa mbadala wa Emmanuel Okwi ambaye taarifa zinasema anaweza akaondoka muda wowote Simba.