Home Uncategorized YANGA WAIPIGIA HESABU CECAFA

YANGA WAIPIGIA HESABU CECAFA


Wakati Simba wakiyatosa mashindano hayo, uongozi wa Yanga umethibitisha kupokea barua ya mwaliko wa kushiriki michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutoka CECAFA.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omar Kaya amesema bado wanatafakari na kufanya tathmini kuona ni faida gani watazipata kabla ya kutoa jibu la mwisho. .

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Azam FC ndiyo timu pekee kutoka Tanzania ambayo imekwishathibitisha kushiriki na imepanga kuanza mazoezi yake rasmi Juni 20 kabla ya kuondoka nchini Julai 4, 2019, kuelekea Kigali Rwanda.

SOMA NA HII  YANGA: HATUNA CHAGUO JINGINE ZAIDI YA KUTAFUTA USHINDI