Mshambuliaji wa klabu ya Zesco United ya Zambia, Lazarous Kambole amekubaliana maslahi binafsi na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika kusini ambayo atajiunga nayo kwa ajili ya msimu ujao, imeelezwa.
Taarifa imesema Kaizer Chiefs italazimika kulipa dau la dola 200,000 ambazo ni zaidi ya milioni 459 za kitanzania kwa klabu ya Zesco kama ada ya usajili kwa mshambuliaji huyo.
Ikumbweke Kambole aliwahi kutajwa kusajiliwa na mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara, Yanga ili kuboresha kikosi chao lakini dili hilo likafeli.
Yanga waliingia kwenye rada za kumsajili mchezaji huyo lakini baadaye kukawa na ukimya ambao viongozi wenyewe walishindwa kuutolea ufafanuzi.