NYOTA wa zamani wa timu ya Barcelona, Chelsea, Inter Milan na timu ya Taifa ya Senegal, Samuel Etoo ameishangaa kuskia Tanzania inashiriki michuano ya Afcon mara baada ya kupita miaka 39.
Etoo amesema kuwa wakati anacheza na Senegal alipata bahati ya kucheza na kikosi hicho mara kadhaa lakini na aliona vipaji vingi kwa wachezaji wa Tanzania.
“Nimeshangazwa kuskia kwamba Tanzania inashiriki michuano ya Afcon baada ya kupita miaka mingi kushiriki kwani wakati nacheza na timu ya Tanzania nilikuwa napambana na wachezaji wenye vipaji.
“Ila kwa kuwa kwa sasa wamepata nafasi ya kushiriki naamini watafanya maajabu kwenye michuano ya Afcon kutokana na aina ya timu waliyonayo pamoja na vipaji ambavyo vipo Tanzania,” amesema Etoo.
Stars kwa sasa ipo nchini Misri ilipoweka kambi ambapo kazi kubwa ya maandalizi imeanza na jana walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri na walipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.