Home Uncategorized MWANTIKA AREJESHWA TAIFA STARS

MWANTIKA AREJESHWA TAIFA STARS


Beki mkongwe nchini David Mwantika amerudishwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichopo Misri kujiandaa na mashindano ya AFCON.

Mwantika amerejeshwa baada ya kuumia kwa Aggrey Morris wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Misri.

Mwantika aliachwa katika mchujo wa mwisho nchini Misri uliofanyika kabla ya kuanza kwa mechi za kirafiki.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 21 nchini humo ambapo Stars itakuwa inashiriki baada ya miaka 39 kupita bila kushiriki.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI