Home Uncategorized Cech arejea Chelsea bila ya ‘Helmet’ yake!

Cech arejea Chelsea bila ya ‘Helmet’ yake!

Mlinda mlango wa zamani wa Timu ya Taifa ya Czech, Peter Cech amerejea tena katika viunga vya jiji la London karibu kabisa na daraja la Stanford kuendeleza makali yake katika soka lakini wakati huu akiwa mshauri wa Ufundi na Uwezo wa klabu ya Chelsea.

Klabu hiyo imemtangaza Cech jana asubuhi ambaye amehudumu kwenye klabu hiyo kwa michezo 494 kama mlinda mlango kabla ya kundoka na kujiunga na Arsenal ambapo alistaafu kucheza soka baada ya kumalizika kwa msimu jana.

Katika utambulisho wa Cech mwenye kichwa cha habari ‘Nguli amerejea’ umesema kwamba kazi kubwa ya Cech kwa sasa si kukaa katikati ya milingoti mitatu lakini sasa itakuwa ni kuzionganisha idara zote za ufundi, kukuza soka la vijana waliopo kwenye shule za mafunzo za klabu hiyo pamoja na kuhakikisha idara zote zinafanya kazi pamoja katika kuisaidia klabu hiyo.

“Nasikia kama heshima kubwa kupata kazi hii, nasema nimepata nafasi nyingine ya kutengeneza mazingira yatakayoinua ufanisi kwenye klabu ili kuyandeleza mafanikio ambayo yamekuwapo kwa miaka 15 iliyopita,” Cech mwenyewe amezungumza hivyo baada ya utambulisho huo.

“Natanguliza hamu ya kujua mengi katika nafasi hii na changamoto mpya iliyopo mbele yangu, na nina amini nitaweza kutumia ujuzi wangu wote wa mpira wa miguu na uzoefu kuisaidia timu kufikia malengo yake huko mbeleni,” amemaliza hivyo Cech ambaye wakati akiwa klabuni hapo ameisaidia timu hiyo kutwaa mataji 15 kwa kucheza dakika 90 bila kufungwa katika michezo 228.

The post Cech arejea Chelsea bila ya ‘Helmet’ yake! appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  WAWILI WA SIMBA KUIKOSA COASTAL UNION LEO