Home Uncategorized MBIVU NA MBICHI ZA ZITAKAZOSHUKA NA KUPANDA TPL KUJULIKANA LEO

MBIVU NA MBICHI ZA ZITAKAZOSHUKA NA KUPANDA TPL KUJULIKANA LEO

MBIVU na mbichi kwa timu za Ligi Kuu Bara (TPL) Kagera Sugar na Mwadui FC kubaki ama kushuka moja kwa moja itajulikana leo baada ya dakika 90.

Kagera Sugar leo itakuwa kibaruani kucheza mchezo wa Playoff na Pamba  uwanja wa Kaitaba huku Mwadui FC ikimenyana na Geita FC uwanja wa Mwadui.

Timu zote mbili zina kumbukumbu ya kutoka suluhu kwenye michezo ya awali hivyo leo ni lazima mshindi apatikane atakayepata nafasi ya kushiriki ligi.

Kama Mwadui na Kagera zitapoteza mchezo wa leo basi itakuwa fursa kwa Pamba na Geita kupanda chati na kupata nafasi ya kushiriki ligi kuu msimu wa mwaka 2019/20.

SOMA NA HII  YANGA YATIA TIMU MORO, KESHO KUVAANA NA MTIBWA SUGAR JAMHURI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here