IMERIPOTIWA kwamba Manchester United wana mpango wa kumsainisha kwa dau la Euro 70 milioni, kiungo mshambuliaji wa Sporting Lisbon, Bruno Fernandes.
United wanashindana na wapinzani wao Manchester City kuipata saini ya nyota huyo mwenye miaka 24 ambaye ni mkali wa assisti.
United tayari wameshafanya mazungumzo na uongozi wa Sporting wakiwa na ombi maalumu kumpata mchezaji huyo haraka iwezekanavyo ili atue Old Trafford.
Fernandes kwa msimu uliopita alifanya maajabu ndani ya kikosi cha Sporting msimu wa 2018/19 ambapo kwenye michezo 53 amefunga mabao 32 na kutoa jumla ya assists 18 in 53.