Home Uncategorized MMOJA TEGEMEO YANGA ANASWA AZAM

MMOJA TEGEMEO YANGA ANASWA AZAM


INADAIWA beki kisiki wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ anawaniwa na mabingwa wa Kombe la Shirikisho (FA), Azam FC ambayo msimu ujao itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Dante amekuwa mmoja kati ya mabeki wa kati wa Yanga waliofanya vizuri msimu wa 2018/19 kwa kushirikiana na beki mkongwe Kelvin Yondani.

Habari za ndani zinadai kuwa nyota huyo anawindwa na Azam pamoja na timu nyingine kutoka nje ya Tanzania.

Hata hivyo, beki huyo inadaiwa bado Yanga inahitaji kubaki naye ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi kwa msimu ujao.

Kwa upande wa Azam kupitia kocha Abdul Mingange, alisema: “Suala la usajili kwa sasa ni mapema kulizungumzia, ripoti yangu nitakabidhi kwa uongozi na kila kitu kitajulikana.”

SOMA NA HII  SIMBA QUEENS IKISHINDA LEO KUTANGAZWA MABINGWA WA LIGI YA WANAWAKE