Home Uncategorized TAIFA STARS: HAKUNA CHA KUHOFIA TUNAKWENDA KUFANYA MAAJABU

TAIFA STARS: HAKUNA CHA KUHOFIA TUNAKWENDA KUFANYA MAAJABU


NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amesema kuwa wanakwenda kufanya maajabu nchini Misri kwa kuwa wanajua wanapeperusha Bendera ya Taifa kwenye michuano ya Afcon nchini Misri.

Stars wamekwea pipa leo kuelekea nchini Misri ambapo wanakwenda kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 21.

Akizungumza na Saleh Jembe, Samatta amesema kuwa kibarua chao kikubwa ni kupata ushindi katika mechi zao kwani watacheza wakiwa ni timu moja.

“Kila mchezaji anatambua kwamba tunakwenda kupambana na timu kubwa na zenye uwezo, licha ya kwamba hauwezi kufananisha uwezo wa mchezaji kama Sadio Mane na mchezaji wetu labda nisema kama Ally Sonso wa Lipuli, ila mwisho wa siku wote ni wachezai lazima tupambane.

“Tumeambiana wachezaji kwamba kazi yetu ni moja kutafuta matokeo na kwenye mpitra lolote linaweza kutokea,” amesema Samatta.

SOMA NA HII  JESHI LA SIMBA V FC PLATINUM