Home Uncategorized WATANO AMBAO TAYARI WAMESHAMWAGA WINO SIMBA KILICHOBAKI NI PICHA ZAO KUACHIWA

WATANO AMBAO TAYARI WAMESHAMWAGA WINO SIMBA KILICHOBAKI NI PICHA ZAO KUACHIWA


Baada ya aliyekuwa kipa wa Yanga, Beno Kakolanya kumwaga wino wa miaka miwili jana na wekundu wa Msimbazi, Simba SC, imeelezwa kuna wengine tayari wameshamalizana na miamaba hao wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa zinasema tayari kuna wachezaji watano ambao tayari wameshamwaga wino lakini picha zao hazijaachiwa mitandaoni.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka Simba zinasema kuwa wachezaji hao ni Ibrahim Ajibu, Serge Wawa pamoja na Shomari Kapombe.

Mbali na watatu hao, wengine wanaotajwa kumwaga wino ni Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ pamoja na Walter Bwalya ambaye anakipiga katika klabu ya Nkana Red Devils ya Zambia.

SOMA NA HII  TFF YATIA TIMU KIGALI KUIPA SAPOTI AZAM FC