Home Uncategorized STRAIKA SIMBA ASIFIA USAJILI WA BALINYA YANGA

STRAIKA SIMBA ASIFIA USAJILI WA BALINYA YANGA


Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mganda, Hamis Kiiza ameusifu usajili mpya wa mshambuliaji, Juma Balinya aliyetokea Polisi ya Uganda.

Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni mara baada ya kupata taarifa za usajili wa Balinya aliyesaini mkataba wa miaka miwili ya kukipiga Jangwani.

Balinya anatarajiwa kuungana na washambuliaji wengine watatu watakaounda safu mpya ya ushambuliaji itakayoongozwa na Maybin Kalengo, Issa Bigirimana ‘Walcott’ na Sadney Urikhob.

Kiiza alisema kuwa anaufahamu uwezo mkubwa wa kufunga mabao alionao Balinya huku akimtabiria mazuri Yanga.

Kiiza alisema, mshambuliaji huyo aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uganda msimu uliopita, kama akipata ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wenzake, basi anaamini atafunga sana Yanga.

Aliongeza kuwa, kikubwa mshambuliaji huyo afahamu anakuja timu yenye presha kubwa ya mashabiki, kikubwa anatakiwa kufanya kazi yake iliyompeleka huko ya kufunga mabao.

“Nafahamu na kuheshimu uwezo mkubwa alionao Balinya katika kufunga mabao, ninaamini atafunga sana mabao kama akiendelea kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wa Yanga.

“Kikubwa ajiandae na presha kubwa atakayokutana nayo Yanga kutoka kwa mashabiki ambao wenyewe wanataka kuona timu inapata ushindi pekee na siyo kitu kingine.

“Ninaamini kama akifanikiwa kukontroo presha hiyo ya mashabiki, basi atafanikiwa katika malengo yake,” alisema Kiiza.

SOMA NA HII  NAMNA YANGA ILIVYOSEPA NA POINTI TATU UWANJA WA MKAPA