Home Uncategorized GADIEL MICHAEL AIBUA JINGINE LA KUSHANGAZA YANGA, SIMBA WATAJWA

GADIEL MICHAEL AIBUA JINGINE LA KUSHANGAZA YANGA, SIMBA WATAJWA


Inadaiwa kuwa beki wa Yanga, Gadiel Michael juzi jioni amesaini rasmi mkataba wa miaka mitatu ya kuichezea Simba kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Gadiel amesaini mkataba huo wa kukipiga Simba ni baada ya mvutano wa muda mrefu kati yake na mwajili wake wa zamani Yanga katika dau la usajli ambalo ni Shilingi Milioni 60 alizokuwa anazihitaji.

Beki huyo anakuwa mchezaji wa tatu kutoka Yanga kusajiliwa na Simba ni baada ya kipa Beno Kakolanya na Ibrahim Ajibu kusaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja.

Meneja wa mchezaji huyo, Jemedari Said alisema kuwa hana taarifa za beki huyo kusajiliwa na Simba baada ya mawasiliano kati yake na beki wake kupotea kabla ya jana jioni kumpikia simu.

Jemedari alisema kuwa beki huyo amempigia simu baada ya kuona taarifa kwenye mitandao amesaini ambazo yeye binafsi kama meneja wa mchezaji huyo zimemshtua.

Aliongeza kuwa, kama beki huyo atakuwa amesaini mkataba Simba atashangaa kwani Yanga ndiyo ilikuwa klabu yake ya kufanya mazungumzo na kuwaahidi viongozi anabakia tena Yanga kitendo ambacho kitakuwa kimkera kama kweli amesaini Msimbazi.

“Mimi kwangu Gadiel kama mwanangu kwa jinsi nilikuwa ninaishi naye na mimi ndiyo niliyempeleka Azam FC na baadaye Yanga tena baada ya Simba kumkataa wakati ninampeleka.

“Nilimpeleka Simba yeye akiwa na akina Bocco (John), Nyoni (Erasto) na Manula (Aishi) nikiwa kama meneja, lakini cha kushangaza timu hiyo ya Simba ilimkataa kwa kusema kuwa wanaye Tshabalala (Mohammed Hussein).

“Baada ya kukatiliwa Simba nikampeleka Yanga nikashukuru wakampokea na kumfanya hivi sasa kuwa katika kiwango cha juu, sasa ninashangaa kuona akiidharau Yanga na ubaya wa hizi timu kubwa hautakiwi kuondoka vibaya.

“Ndani ya wiki hii Gadiel sikuwa na mawasiliano naye mazuri na ninaomba nijitoe kwenye hili kama kweli amesaini Simba na hii ya kusaini itakuwa na ukweli kwa sababu simuelewi huyo dogo, nitafute baadaye usiku (jana) nitakuwa na majibu mazuri kwani ninakwenda kuonana naye na ninaomba nisieleweke vibaya kwa Yanga,” alisema Jemedari.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA TANZANITE KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA AFRIKA KUSINI MICHUANO YA COSAFA