UONGOZI wa klabu ya Yanga umewataka mashabiki na wadau wa Yanga kuacha vitendo vya kuihujumu nembo ya Yanga kwa kuchukua bidhaa feki kwani tayari wamepata dawa ya kudhibiti vitendo hivyo.
Akizungumza na Saleh Jembe makamu mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa wamejipanga kudhibiti wapigaji wote msimu ujao bada ya kumpata mzabuni mpya ambaye ni GSM.
GSM inamilikiwa na bilionea kijana Said Ghalibu ambaye anamiliki maduka mbalimbali ya kuuza nguo nchini na nje ya Tanzania.
“Vigezo ambavyo tuliwapa ilikuwa ni pamoja na uwezo wa kutengeneza jezi kwa wingi zenye ubora,kujenga duka makao makuu,gharama zao, faida kwa Yanga ni ipi hivyo atakayehusika kuuza jezi zenye nembo ya Yanga kuanzia wiki ya wananchi ni GSM.

“Wale ambao wanaihujumu Yanga kwa kutumia bidhaa feki ni muda wao wa kuacha na kuipa sapoti Yanga kwa kupata bidhaa bora na zenye uhakika, kwa watakaokiuka hatua kali juu yao zitachukuliwa.
“Mpango ni mkubwa na wa uhakika hivyo baada ya muda makao makuu ya Yanga kutakuwa na duka la bidhaa halisi za Yanga,” amesema.