MWEKEZAJI wa Simba, Mohamed Dewj, leo ameandika ujumbe mfupi ambao umeacha maswali mengi kwa mashabiki na wadau wa soka kutaka kujua maana ya maneno hayo.
Mo amekuwa na kawaida ya kuandika ujumbe mfupi kwenye kurasa zake ambao umekuwa ukiacha maswali mengi kwa wanaomfuatilia kwa sasa.
Kupita ukurasa wake wa Instagram, Mo ameandika namna hii : “Uongo unapanda kwa lifti.Ukweli unapanda kwa ngazi,”.
Kauli hiyo imeamsha hisia za wadau wengi wakitaka ufafanuzi zaidi kwani maneno ni mafupi na hayajatolewa ufafanuzi zaidi.