UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kwa sasa hesabu kubwa ni kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.
Azam FC imerejea nchini baada ya kushindwa kutetea kombe la Kagame leo inaanza mazoezi ya kujiaandaa na msimu ujao.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa wamekubali kushindwa kutokana na ushindani.
“Tumepoteza kombe letu ila tumepambana, kwa sasa ni muda wa kujipanga kwa ajili ya michuano ya kimataifa,” amesema.
Azam FC walikuwa ni mabingwa watetezi wamelipoteza kombe hilo kwa kufungwa bao 1-0 na KCCA ya Uganda.