Home Uncategorized NYOTA SABA KUJIUNGA LEO NA TIMU YA TAIFA, MMOJA TAARIFA ZAKE HAZIFAHAMIKI

NYOTA SABA KUJIUNGA LEO NA TIMU YA TAIFA, MMOJA TAARIFA ZAKE HAZIFAHAMIKI


KOCHA msaidizi wa timuya Taifa, Juma Mgunda amesema kuwa leo wachezaji saba waliokuwa nchini Afrika Kusini watajiunga na Timu ya Taifa kufanya mazoezi ya kujiaanda na mchezo dhidi ya Kenya Julai 28 uwanja wa Taifa huku nyota mmoja taarifa zake zikiwa hazifahamiki.

Wachezaji wa timu ya Taifa walianza kambi Julai 21 ikiwa ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Kenya isipokuwa wachezaji nane hawakuripoti kambini kutokana na sababu mbalimbali.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wamepata taarifa kwamba wachezaji wataripoti kambini mapema na kuanza mazoezi.

“Programu ya asubuhi itawahusu wachezaji waliokuwa nchini Afrika Kusini na wataanza mazoezi mara moja kwa kuwa hatuna muda wa kupoteza kwa sasa na siku zimebaki chache.

“Tuna imani ya kufanya vizuri kwa kuwa kikosi chetu kina morali hivyo wakiungana na wachezaji wengine kitazidi kuimarika,” amesema.

Wachezaji ambao wanatarajiwa kuanza mazoezi leo ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, John Bocco, Hassan Dilunga, na Aish Manula huku Idd Chilunda taarifa zake hazifahamiki. 

SOMA NA HII  KOCHA KATWILA AIPIGA BONGE MOJA YA MKWARA NAMUNGO