Uncategorized

SERIKALI YARUHUSU WACHEZAJI KUMI WA KIGENI KUSAJILIWA BONGO, MASHARTI YAKE SI MCHEZO

admin July 26, 2019 2:21 pm

HARRISON Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, amesema kuwa kwa sasa ni ruksa wachezaji wa kigeni kusajiliwa kumi kwa timu za ndani.

Matokeo haya ni baada ya Dk.Mwakyembe kukaa na uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuzungumza kwa kina juu ya suala hili ambalo awali serikali ilizuia.

Mwakyembe amesema kuwa kuna vigezo vya msingi ambavyo vinapaswa viangaliwe kabla ya wachezaji kusajiliwa.

“Vigezo ambavyo tumekubaliana na TFF ni pamoja na kuona kwamba wachezaji wa nje wawe wanatoka kwenye timu ya Taifa huko wanakotoka na pia kutakuwa na vigezo vya kujiridhisha na ubora wao.


“Wachezaji wa ndani pia watakaosajiliwa wanapaswa wapewe nafasi sio wanaishia kusugua benchi kwani tunataka kuwa na timu bora ya Taifa,” amesema.

BREAKING: BOCCO ATEULIWA KUWA NAHODHA WA TIMU YA TAIFA DILI LIKIKAMILIKA LUKAKU KUSEPA UNITED MAZIMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply