SERGIO Arguero,mshambuliaji wa Manchester City alijiunga na klabu hiyo Julai 28, 2011 akitokea Altletico Madrid na rekodi yake ni tamu.
Mpaka sasa amecheza jumla ya michezo 338 huku akipachika jumla ya mabao 231.
Aguero ametoa pasi za mwisho 69 kwa upande wa kabatini amebeba makombe manne ya Ligi Kuu England sawa na yale ya League Cup na ana ngao za jamii mbili huku FA ikiwa ni moja.
Pia ana tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa uingereza akiwa ameibeba mara sita pia ana tuzo mbili za mchezaji bora wa England (PFA).







