MBRAZIL anayekipiga Simba ambaye ni kiraka anacheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji Gerson Vieira amesema kuwa ni furaha kuwa ndani ya Simba kwa sasa.
Vieira amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya kikosi cha Simba kwenye usajili wa dirisha kubwa akitokea timu ya ATK FC ya India kwa sasa yupo na timu nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
Mbrazil huyo amesema :”Wachezaji wenzangu walinipokea vizuri jambo linalonipa furaha na ninafurahi kuwandani ya Simba.
“Tupo na Kocha mwenye uwezo mkubwa hivyo tunaamini tutafanya makubwa pia na kila mmoja yupo vizuri, na tuna kocha mwenye uwezo mkubwa,” amesema.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.