Uncategorized
MANCHESTER UNITED KUMKOSA BAILLY KWA MUDA WA MIEZI MITANO
OLE Gunnars Solskajer, Meneja wa Manchester United amethibitisha kuwa beki wake kisiki Erick Bailly atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi minne mpaka mitano.
Bailly alipata majeraha hayo kwenye mchezo wa kirafiki wa michuano ya ICC dhidi ya Totthenham wiki iliyopita wakati United ikishinda kwa mabao 2-1.
Nyota huyo mwenye miaka 25 atakuwa chini ya uangalizi wa madaktari mpaka pale atakaporejea kwenye ubora wake.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.